Monday, September 29, 2008

AUAWA KISHA ACHUNWA NGOZI BONGO


Huku watu wakiwa bado wapo roho juu kuhusu mauaji dhidi ya jamii ya watu wenye ulemavu wa ngonzi(albino) kutokana na imani za kishirikina.Tukio jingine limetoa mwezi huu huko Shinyanga, bw Lifa Dogani ameuawa kisha kuchunwa ngozi.

Sababu ya wauaji kutekeleza zoezi ilo ni lengo la kujipatia ngozi ya binadamu na kwenye kuiuza kwa wafanyabiashara ya madini alamasi,Mwadui.


Wahusika wote wa tukio wanashikiliwa na polisi.

Nakumbuka tabia ya uchunaji ngozi ilianza na kupotea.Sasa imerudi.Yaani jamii yetu inahitaji sana kuelemishwa jinsi ya kujikwamua na 'ugumu' wa maisha.Waelimishwe kuhusu imani za kishirikina kuwa haziwezi kuwakwamua kimaisha.

Inasikitisha sana.Ulaya wanauwana kwa sababu ya technolojia(watoto wanamiliki siraha).Nyumbani tunauwana kwa sababu ya imani za kishirikina na 'ujinga'.

Mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi.Amina


Naamini..Tutafika tu


habari zaidi bofya HAPA

5 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kaka Edo, kwa kweli inasikitisha sana kwani kila siku ukiamka vifo vya aina mbalimbali na vituko vya aina mbalimbali. Inaogopesha sana kuishi pia watu tutaogopa hata kutoka nje maana ukitoka tu nje basi wasiwasi tu au hata kama kunapigwa hodi unaogopa hata kufungua mlango. Najiuliza wao watafanya nini na hiyo ngozi. Unajua huo mtindo wa kuchuna ngozi ulikuwepo mwaka 2001 Peramiho nilikuwa sisafiri kabisa. Nasema pia marehemu astarehe kwa amani. Amena.

Matty said...

Ohh God what a shame is spreading in Tz!RIP ndugu!
I pray to God that its better the killer wouldn't stay long life, they suppose to enjoy the torment!
TUTAFIKA!

Anonymous said...

kweli ni hali ya kusikitisha sana watu wangu.

ndio hivyo tena..kwenye watu kumi..binadamu mmoja

james kiguu

Anonymous said...

hivi inakuwaje mtu unapata ujasiri wa kumchuna binadamu mwenzako bila hata hofu au dhamira.

binafsi hata kuchuna mbuzi tu mwili unasisimka..sasa hao wanaotoa roho za ndugu zetu sijui wakoje.

huu sio ubinadamu yaani sasa hivi bora ukutane na simba ujue moja kuliko kukutana na mtu usiku

MKOKOZI MWANZA said...

RIP ..pole kwa ndugu jamaa na marafiki wa marehemu.

natumaini sheria itachukua mkondo wake.

inasikitisha saaaana