Monday, October 13, 2008

CHADEMA WASHINDA UCHAGUZI WA TARIME


(Bendera ya CHADEMA)

Katika kile kilichoonyesha hali ya kukatishwa tamaa na Chama Cha Mapinduzi na sera za kukumbatia Ufisadi.Wananchi wa Tarime wameachagua kwa mare nyingine kukinyima kura Chama Cha Mapinduzi licha ya kugawa takrima za kofia,kangha,fulana,pesa n.k.

Wananchi wa Tarime wamewachagua wagombea nafasi ya Ubunge na Udiwani wote kutipitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA na kuacha CCM na vyma vingine vikiambulia Patupu.

Uchaguzi huo umekuja baada ya kifo cha aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo marehemu Chacha Zakayo Wangwe.

Pongezi wananchi wa Tarime,tume ya uchanguzi kwa usimamizi mzuri wa kura.

Huo ni ushindi si wa Chadema bali wananchi na Demokrasia.Ni wakati sasa wa kusahau tofauti za CCM na Chadema na kujenga jimbo lenu.

Hongera tena kwa washindi.CCM inajifunza nini kutoka Tarime?

2010 inakaribia..Tutafika tu


MATOKEO

UBUNGE:
CHADEMA - 34,545
CCM - 28,996
NCCR-MAGEUZI - 949
DP - 305

UDIWANI
CHADEMA - 4,820
CCM - 3,239
TUTAFIKA TU

0 comments: