(Picha kutoka blog ya DA CHEMI)Watoto 19 wamefariki dunia baada ya kutokea mkanyagano kwenye ukumbi wa Disco wakati wa sikukuu ya Idd huko Tabora.
Watoto hao wamakufa na wengine kujeruhiwa walipokuwa kwenye "Disko Toto" wakati wa MCHANA.Sababu ya vifo hivyo ni watoto kukosa hewa( Suffocation),kutokana na ukumbi kuchukua idadi ya watoto zaidi ya 400 ambayo ni idadi kubwa zaidi.
Kwa tamaa ya PESA..kutojali sheria na kutosimamia sheria yametupelekea hapa.
Mkaguzi wa majengo anasema ..Ukumbi huo ulijengwa kwa ajili ya mikutano na SI DISKO.Hii imekaaje wenzangu.INAUMA SANA SANA.
Mwenyezi Mungu azipumshishe roho za marehemu mahala pema.Amina.N awajalie moyo wa subra ndugu,wazazi na marafiki.Amina
Maeneo ya wazi kwa ajili ya burudani kwa watoto mengi yalishavamiwa.Na yaliyopo hajaendelezwa.Hivi kweli serikali kwa kodi inayokusanya inashindwa hata kutenga kiasi kidogo cha pesa kwa ajili ya mabembea na vitu mbalimbali kama sehemu ya mikusanyiko ya watoto wetu.
Inauma sana.
Habari zaidi bofya HAPA



2 comments:
Jamani kwanza habari za siku. Kwa kweli ndiyo inauma sana. Halafu hii ni kweli tamaa ya pesa ni kama daladala mwaka jana nilitamani kulia jinsi daladala inavyojaza watu. Namwomba mungu kusitokea kitu kibaya. Marehemu wastarehe kwa amani.
Inauma sana!Mungu awalaze mahali mema peponi!
Post a Comment