Monday, June 21, 2010

UZINDUZI WA TAWI LA CCM HELSINKI FINLAND

MABADILIKO YA UKUMBI NA TAREHE!

KUTOKANA NA SABABU NJE YA UWEZO WETU TUMERUDISHA NYUMA SIKU MOJA YAANI ALHAMISI BADALA YA IJUMAA AMBAYO NI SIKUKUU MUHIMU HAPA FINLAND (MID-SUMMER-JUHANNUS) KUTAKUWA NA SHIDA YA USAFIRI.

PIA KUTOKANA NA KUPOKEA EMAILS NYINGI ZA WASHIRIKI KAMATI YA MAANDALIZI IMECHUKUA UKUMBI MKUBWA NA WA KISASA PALE PALE KATIKATI YA JIJI LA HELSINKI-RAVINTOLA KAISANIEMI (THE HOME OF AFRICAN NIGHT) KAISANIEMENTIE 6.

TAREHE: ALHAMISI 24.6.2010
MUDA: 18.00pm -23.30pm
BAADA YA MKUTANO: KUTAKUWA NA BURUDANI YA NYIMBO ZA KINYUMBANI TU NA DJ. ALTUNEZ.

KWA WALE WANAOJISIKIA KUJA KUFAHAMIANA NA WATANZANIA WENZAO, TUTAKUWA NA MAZUNGUMZO YA PAMOJA NA BAR KUWA WAZI KWAAJILI YA VINYWAJI BAADA YA MKUTANO 21:00.

NB: WANAKAMATI WANAFANYA MAWASILIANO NA BALOZI WETU WA SWEDEN AU MWAKILISHI WAKE ILI AWEZE KUWA MGENI RASMI KWAAJILI YA UFUNGUZI.

2 comments:

Anonymous said...

hivi nyinyi hamuoni ccm hiyohiyo ndo inayowaacha ndugu zenu kule vijijini bila maji ya kunywa na wakinamama wa kule wanabebwa na baiskeli wakiwa na uchungu wa kujifungua wao magari yetu wamepaki bar.

edwin,hautoniona tena kwenye blog yako.kumbe umeubeba upuuzi wa ccm na kwenda kuushabikia finland.kumbe na wewe ni mtu wa kujipendekeza hivi?najuta kukujua.

Anonymous said...

Na mimi naungana na anony wa hapo juu. Nilidhani mtu wa maana kumbe loh. Sitaingia tena kwenye blog yako, huna uchungu na sisi.