Friday, December 9, 2011

Hongera Tanzania miaka 5O uhuru..Changamoto bado nyingi.

Mtanzania akiwa amebebwa na "ambulance" akipelekwa kupata tiba(iwapo itapatikana) miaka 50 baada ya uhuru.

Taifa changa duniani Sudani kusini ambalo halijasherekea hata mwaka mmoja wakitumia NJIA mbalimbali ili kuhakikisha wananchi wake wanapata huduma ya afya hadi vijijini..Tunajifunza nini?

Leo nchi yangu imetimiza miaka 50.

Hongera sana kwa watanzania wote popote walipo.Kuna "mengi ya kupongezwa" kwa hapa tulipo lakini naamini hata WAO wanajua tunamengi yalio ndani ya uwezo wetu jamii au viongozi hawajitimiza wajibu wao mpaka kupelekea hapa tulipo.

Chukulia mfano hizo picha hapo juu.Tunao mabwana afya hadi ngaji ya kijiji lakini unamkuta hana vitendea kazi mfano hata jinsi ya kumfikia mwananchi.Lazima wadau wote,serikali,mtu mmoja mmoja tusimame kwa sauti na vitendo kuhakisha tunasherekea kwa sababu za msingi.

Bado tunasafari ndefu tulistahili kuwa mbali zaidi ya hapa.Na tunastahili kuwa mbali zaidi ya hapa.

Hongera Tanzania ingawa badi unachamoto nyingi..Rushwa,miiko ya maadili/utawala bora matumizi mazuri ya raslimali na kodi za watanzania.

Tutafika tu

0 comments: