Friday, December 23, 2011

Tanzania Broadcasting Corparation(TBC) WEBSITE-R.I.P

Bw Danstan Tido Mhando

MWAFRIKA wa kwanza kuongoza Idhaa ya Kiswahili ya Radio ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC), Danstan Tido Mhando,

Bw Tido Mhando baada ya kustaafu BBC Swahili akarejea nyumbani na kuwa mkurungezi mtendaji wa TBC(Tanzania Broadcasting Cooperation) kufanya MAPINDUZI makubwa.TENDA WEMA NENDA ZAKO,,mbali na yote hayo serikali iliamua kutomuongezea mkataba wa kazi na kumuweka pembeni.

Wachambuzi wa mambo ya habari wanaamini hayo yalifanyika kwa kile kilichoonekana serikali kutofurahia jinsi TBC iliyotoa fursa sawa kwa vyama vyote vya siasa wakati wa uchanguzi 2010.

Bw Tido Mhando kwa kuwa ni mtu anaye heshimika ktk tansia ya habari,kwa sasa habari za kuaminika amechukuliwa na Al jaazera swahili ambayo inatarajia kwenda hewani kuanzia 2012.
Popote alipoa aliondoka kama shujaa aliyetimiza wajibu wake.Hivyo ndivyo ninavyoamini.

Bw. Clement Senzota Mweta Mshana.

Bw.Clement Mshana alikuwa mkurugenzi wa Idara ya habari(MAELEZO).

April 21,20011 Rais Jakaya Kikwete alimteua Bw Mshana kuchukua nafasi ya Bw Tido Mhando kuwa mkurugenzi mtendaji wa shirika la utangazaji tanzania (TBC).

KAZI aliyofanya Bw Mshana ni KUHARIBU yale mazuri yaliachwa na kurejea YALEE YALEE KUHARIBU kama tulivyoweza kuharibu mashirika ya umma kama vila KAMATA ,UDA n.k

Leo naangalia habari kupitia TBC nakuta last update website ilikuwa november 5..ukitaka kuamini click www.tbc.co.tz

BW Mshana usilale,jifunze kutoka kwa majirani tusiende nchi za mbali.

RWANDA ( Rwanda Berau of Information and Broadcasting)
KENYA ( Kenya broadcasting corporation)
UGANDA ( Uganda broadcasting corporation)
TANZANI ( Tanzania broadcasting corporation) aibu aibu usipoteza muda kuclick


SWALI?
1.Hivi ni kweli hatuna watu wenye utalaamu wa kuupade website?Kama tunao tatizo nini?


2.Sasa TBC hiyo website ya kazi gani?tupo serious kweli?


Mungu ibariki Tanzania..

TUTAFIKA TU.






2 comments:

Anonymous said...

hii ndi tanzania kaka ..watu huku tupo mitaani hatuna ajila,wanabeba bila sifa mwisho wa siku mambo ya aibu..

Anonymous said...

tangu kaondoka tido ata sina muda wakupoteza kuangalia hiyo Tanzania brainwash corperative..


ipo siku patachimbika..nimeangalia hiyo site aisee ni nuoumer kaka