
Jumapili ya jana waasi wanaongozwa na General Laurent Nkunda wameteka mji Kibumba mashariki ya Congo.Na kupelekea majeshi ya serikali kukimbia eneo ilo.
Kibaya zaidi Kingozi wa vikosi vya kulinda Amani naye kajiuzuru jana baada ya kushikiria nafsi hiyo kwa majuma manne tu.
Bosi huyo anajiuzuru huku wananchi wakiwalilia kwanini wameshindwa kuwasaidia kuwathibiti waasi.
Zaidi ya watu 200,000 wameshayakimbia makazi yao.Habari zaidi unaweza kusoma kwa kubonyeza HAPA.
Bado utakumbuka Genocide 1994 ya Rwanda ..walinda amani wanaonekana sasa kuanza kujitoa kimya kimya?
Poleni watoto,wakina mama na wote mnaoteseka na vita za kila siku
Safari yetu ni ndefu ..sasa tutafika kweli?
7 comments:
Sikiliza Kaka Edo. Swali ni kwamba kuna kiwanda cha silaha kinachotengeneza hayo mabomu na bunduki? Kama watu hawafanyi kazi wanapata wapi pesa za kuwalipa hao maaskari? Jiulize kama huyo Nkunda aliweza kufanya interview na Anderson Cooper kwanini ulimwengu ushindwe kumkamata? Ulimsikia Inno Galinoma katika "Vita Vya Panzi"? Labda nikupe mstari wa Nasio Fontaine alioimba kwenye wimbo wake Babylon You Doom aliposema "YOU BUILDING MORE BOMBS AND GUNS YET BABIES ARE DYING FOE HUNGER, WE ARE THE VICTIMS OF YOUR OPPRESSIONS. BLOOD OF THE INNOCENT THAT YOU SLAUGHTERED IS UPON YOUR HANDS. YOU GAVE THE GUNS, YOU SET THE FIGHT, YOU SIT ASIDE AND WATCH THE SLAUGHTER"
Blessings
Inasikitisha sana!:-(
Simon kweli hali si nzuri kabisa.
Mutwiba nashukuru kwa mchango wako mzuri.
Kweli hii vita kuna watu wamesimama pembeni wakiangalia tukiuana.
Ila ipo siku ukweli utajulikana.lUCKY Dube aliimba Crime doesn't pay..
Mama kama mama wa kiafrica anaumia siku zote, inauma sana kuna wakati huwa najiuliza hv kwanini?jibu sipati.
Mungu wangu nakuomba utupe nguvu na kutulinda sisi wanawake!
chukua 5 Mutwiba umeongea point, hawa wakubwa they are stupid kabisa wananiboa sana!
Thanx alot Matty. Respect to you too.
Mutwiba
Ndugu yangu ukijitahidi kuvaa viatu vya huyo mama ndio utajua jinsi gani anavyoteseka.
Ukizingatia sio sinema ya hollywood ila ni hali halisi inamtokea.
Kilio chake ni kwa ajili ya aliyemgongoni na tumbuni kwake achilia mbali yeye mwenyewe hajui hata anapokimbilia kuna usalama gani.
Hana passport ya kukimbia nchi,wala pesa.
Hana kifaru cha kujilinda.
Hana lolote jema analopata kati ya serikali iliyomtelekeza au waaasi nwanaotafuta roho yake.
Poleni sana wakina mama na watoto duniani koote mnaoteseka kutokana na mamuzi ya watu wachache.
Ipo siku yote yatakwisha.
Tutafika tu
Post a Comment