Friday, December 30, 2011

MWANAHABARI JOHNA NGAHYOMA AFARIKI DUNIA -RIP

Enzi za uhai wake mwandishi mkongwe marehemu John Ngahyoma(kushoto) akifanya mahojiano.

Mwanahabari mkongwe wa shirika la utangazaji BBC bw John Ngahyoma ameaga dunia leo asubuhi jiji Dar es salaam.

Enzi za uhai wake aliwahi kufanya kazi katika kituoa cha Radio Tanzania Dar es salaaam(RTD),ITV na baadaye TVT mpaka mauti yanamfika alikuwa BBC.

Msiba upo nyumbani kwa marehemu Tabata jirani na nyumba ya Danny Mwakiteleko.

Taarifa imetolewa na katibu mkuu jukwaa la wahariri BwNeville Meena.

Pole Glorie Ngahyoma pamoja na ndugu jamaa na marafiki.Mwenyezi Mungu awatie nguvu ktk kipindi hiki kigumu mnachopita.

Mwenyezi Mungu aile roho ya marehemu mahala pema peponi.AMINA

No comments: