Pichani jana nikiwa mji mkuu wa Jamuhuri ya Czech, Prague.
Salaam kutoka Jamuhuri ya watu wa Czech. Nilianza kublog mwaka 2007 hadi 2014. Baadaye niliamua kupumzika kublog. Nilipendelea kutuma picha na habari fupi, ikiwa ni sehemu ya kutumia taaluma yangu ya habari niliyoipata chuo kikuu cha SAUT mwanza na Tampere,hapa Finland.
Baada ya mapumziko ya tangu Juni 2014, ikiwa ni miaka miwili na miezi saba, leo nimeamua kurejea kwenye hili 'libeneke' kama anavyoliita nguli wa blog ISSA MICHUZI .
Mengi yamejitokeza, blog nyingi zimezaliwa na kufa ktk kipindi hiki. Sisi tulipoanza ilikuwa lengo kuu ni kuhabarisha, kabla kuwa 'chanzo cha kipato'.
SASA NAREJEA TENA KWENYE HII MEDANI. TUTAFIKA TU
Kama ulivyo msemo mkuu wa hii blog TUTAFIKA TU.
Wasalaam
Edo Ndaki
edondaki.blogspot.com
Prague, Czech.
17-02-2017
2 comments:
AFadhali uredi bwana maana wanablogg wengi wa miaka ile hawapo...Binafsi nakukaribisha na kukupokea kwa mikono miwili pia kwa furaha tele jirani yangu...kweli ni kipindi sasa ...habari za tangu mwaka juzi:-)
Asante sana dada Yasinta. hongera sana kwa kuweza kudumu na kwanguvu zote
Post a Comment