Friday, May 9, 2008

HIVI TUPO UHURU KWELI?

Pichani nikiwa kwenye lilipokuwa soko la watumwa Zenj june,2005.Mtoto mwenye kaptula ni "uncle" wangu.

Historia ni mwalimu. Tulinde vivutio vyetu na kufisha ujumbe kwa vizazi na vizazi. Ukifika Zanzibar , Bagamoyo na mikoa ya Pwani utakutana na historia kubwa na masalio ya kale.

8 comments:

Simon Kitururu said...

Tatizo ni elimu na umasikini.
Mwenye visenti anaweza kucheza na mawazo ya wasio na data kirahisi kuliko watu wafikiriavyo, kama wahusika hawana data za kutosha halafu wana njaa na Mfisadi anagawa ubwabwa.

Anonymous said...

Yaani Simon! unayosema ni ya kweli kabisa.Maana Chenge unaambiwa kila kijiji alichopita..ng'ombe walichinjwa.

Ina maana huo umati ulijitokeza kumpokea wengi wao kutokana na ugumu wa maisha anaona bora anaende kwenye tukio japo naye apate japo msosi.
Inasikitisha sana

Anonymous said...

Wengi kazi yao kufata mkumbo.na wengine ndio hivyo tena hata taarifa kamilia hawana.Hivyo wakidanganywa kidogo tu wanakubali

Anonymous said...

Edo unajua inaumiza sana kuona watu wanazidi kubaki katika utmwa wa kifikra.

Unajua huklu bongo walio wengi ,wamezoea kunyanyaswa,mateso.

Wameshakata tamaa na maisha.ndio maana kila siku afadhali ya jana.

Watu wanaona ..hata wasiopoenda kumpokea chenge..watakaa tu kijiweni hivyo mtu anaona bora aende labda anaweza kupata chochote huko.

Innocent

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yaani ndugu zangu yoote mnayosema ni ya kweli kabisa.

Watu nyumbani walio wengi bado wapo usingizini.Na wale walio amka wanaogopa kuongea.Maana wanajua MWENYE nguvu ndiye kashikilia mpini na sisi masikini tumeshikilia kwenye makali.

Mwisho wa siku watu wanazidi kukata tamaa na kuondoa,imani kwa viongozi wao.Hapo sasa ndio tutakuwa tumefika pabaya.

Ila kila lenye mwanzo lazima liatkuwa na mwisho tu.

Anonymous said...

masai hapo ulikuwa unajaenda Finland nini?Naona ka rangi kako keusi kweli yaani kanataka kuelekea blu..aaaa aaaa

Ila bonge la kumbukumbu..mambo ya zenj

Zaka-Arusha

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Si unajua tena jua la bongo Zaka.

Ukichanganya na tukamera twa vijisenti vichache..kaflash kenyewe kimeo..battery feki ya chini..aa aaa kitu ukichukua kwa mdosi anakwambia kitu "jinuini" nenda dunia nzima hupati...aaa

karibu sana..mpe hi DAMAS LOINA

Anonymous said...

unapoangalia au kufuatilizia siasa katika nchi ziizoendelea ni kwamba wanachi wengi wameelimika na wanaojua haki zao na uongozi ni kuwajibika kwa wanachi wanaokuweka madarakani na wakiona huwafai wanakutupia mbal bila kujali una degree ngapiau umetokea wapi watakolia ni familia yako tu.
afrika siasa ni ya wenye kusoma na wengine ni wajinga tu wanafuata kama wanasiasa wao wanavyotaka kwa hiyo wanasiasa wamakua nima-elite katika nchi na ndio maana utakuta patashika ya siasa ipo miji mikuu tu lakini vijijini hakuna mwamko wowote ule ni ujinga mtupu na umasikini.kama hatutopata kiongozi kama mwalimu nyerere hawa waliokuja na watakaokuja ni wezi tu hawana patriotisim wala kuwapenda wanaowatawala.