Friday, February 17, 2017

TAARIFA YA MSIBA STOCKHOM SWEDEN: BW SALVATORY RUTAHINDUKA KAMALI (R.I.P)

Marehemu Bw Salvatory Rutahinduka Kamali (RIP)

Jumuiya ya watanzania Sweden, inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yetu mpendwa SALVATORY RUTAHINDUKA KAMALI kilichotoea February 16, 2017 kwa kuangukiwa na gari akiwa kazini Sweden.

Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa hospitali kwa uchunguzi, mara polisi watapokamilisha taratibu zao mtajulishwa taratibu za wapi kukutana na jinsi kuchangisha rambirambi kwa ajii ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi.

Marehemu hana ndugu aliyepatikana hapa Sweden hivyo kwa maelezo zaidi unaweza wasiliana na 
+ 46 70-642 43 99  SKOLA
  + 46729265552  NORMAN
 
TAFADHALI SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WENGINE NI MSIBA WETU NA MARAFIKI ZETU.
Pumzika kwa amani. Amina

Leo nairejesha EDONDAKI.BLOGSPOT.COM baada ya mapumzika ya miaka miwili na nusu..NIPOKEENI

Pichani jana nikiwa mji mkuu wa Jamuhuri ya Czech, Prague.

Salaam kutoka Jamuhuri ya watu wa Czech. Nilianza kublog mwaka 2007 hadi 2014. Baadaye niliamua kupumzika kublog. Nilipendelea kutuma picha na habari fupi, ikiwa ni sehemu ya kutumia taaluma yangu ya habari niliyoipata chuo kikuu cha SAUT mwanza na Tampere,hapa Finland.

Baada ya mapumziko ya tangu Juni 2014, ikiwa ni miaka miwili na miezi saba, leo nimeamua kurejea kwenye hili 'libeneke' kama anavyoliita nguli wa blog ISSA MICHUZI .
Mengi yamejitokeza, blog nyingi zimezaliwa na kufa ktk kipindi hiki. Sisi tulipoanza ilikuwa lengo kuu ni kuhabarisha, kabla kuwa 'chanzo cha kipato'.

SASA NAREJEA TENA KWENYE HII MEDANI. TUTAFIKA TU

Kama ulivyo msemo mkuu wa hii blog TUTAFIKA TU.

Wasalaam 

Edo Ndaki
edondaki.blogspot.com

Prague, Czech.
17-02-2017

Monday, June 23, 2014

BONGO FC (Finland) WAISAMBARATISHA NIGERIA 4- 2

Timu ya watanzania Bongo FC yenye maskani yake Finland.Picha baada ya pambano lake na timu ya Nigeria na kufanikiwa kuzoa ushindi mnene wa mabao 4-2.

Bongo FC miongoni mwa timu kongwe na kielelezo cha uwakilisha wa Tanzania kwenye ukanda wa nchi za 'scandnavia'.

Bongo FC imefanikiwa kuanza kampeni yake ya msimu wa majira ya kiangazi kwa kucheza michezo miwili.Mchezo wa kwanza waliifunga timu Ethiopia magoli  5-3 na mwishoni mwa juma kuifunga timu ya Nigeria 4-2.

Wafungaji wa magoli akiwa Mwita Chacha , Bakari Salehe, Tonny aka Diego Simeon..Hizi ni salaam kwa ndugu zetu wa Sweden Kilimanjaro FC...

Hongera Bongo FC

Tutafika tu

Friday, May 30, 2014

WORLD VILLAGE FESTIVAL 2014-HELSINKI FINLAND

Baadhi ya watanzania waishi jiji la Helsinki Finland picha ya pamoja muda mfupi baada ya maandalizi ya banda la jumuiya ya watanzania na finland  (STS) kwenye maonyesho ya "World Village Festival'

Kutoka kulia Noeli Makumuli mjumbe wa bodi , msaani wa kimaitaifa wa Raggae kutoka Tanzania Jhikoman pamoja na Edo Ndaki Mwenyekiti wa Finland Tanzania Friendship society - STS

Picha huongea maneno zaidi ya elfu moja.Hakika banda la wawakilishi wa Tanzania lilifana na kutembelewa na wageni wengi.

Kutoka kulia bw Fidelis Tungaraza akitoa ufafanuzi kwa mgeni aliyetembelea banda huku bw Edward Mtafungwa na Noel Makumuli viongozi wa bodi ya STS wakiendelea kuhabarisha wageni mambo mbalimbali yahusuyo Tanzania.

Mark Mhekwa kati ya watanzania waliopata muda wa kutembelea banda la maonyesho la jumuiya ya watanzania na wafini.

Naam,Moudy alimletea binti yake kumnunulia vitabu pamoja na cd za kiswahili ili aweze kujifunza lugha ya baba.Safi sana.

"One loveeeeeeeeeee" kutoka kushoto msanii wa muziki wa Raggae kutoka Bagamoyo Tanzania Jhikoman, nguli Popo pamoja na makamu mwenyekiti wa jumuiya Ilona Tika.

'Karibu Tanzania' nilitembelea na mwanafunzi ninayesoma naye chuo kimoja .Hakuondoka hivi hivi alivutiwa na kitabu chetu cha 'KARIBU TANZANIA'

Wadau wa jiji la Helsinki..Hii picha naomba msaada wa caption :D

Sunday, March 30, 2014

TUTAFIKA TU: NAAM!! NIMEPATA NGUVU YA KUREJEA KUBLOG TENA!

   Edo Ndaki pichani nikiwa kwenye moja za 'SAFARI' za hapa napale jiji, Tampere Finland.


Habari za tangu mwaka jana 2013.Hakika nilihadima kwenye medani ya 'kublog'. Majukumu ya hapa na pale yalinifanya nikose fursa ya kuwasiliana na blog wenzangu na hata wasomaji wangu.

Nafarijika kila kukicha nionapo 'indastri' hii inavyukua. Nawapongeza marafiki ambao kwa miaka nenda rudi wamekuwa na nguvu ya kuendeleza libeneke kwa miaka kadhaa sasa.  Hakika tambueni chango wenu ni mkubwa,endeleeni bila kuchoka.

Kama ilivyokauli kauli mbiu ya blog hii "TUTAFIKA TU" basi naamini tutafika tu.Nitaendelea kuwaletea  matukio mengi zaidi yanayotokea huku niliko Ufini pamoja na majirani zangu huku barani Ulaya yenye manufaa kwa wadau wote.

Asante kwa kunisoma.

TUTAFIKA TU.

Wednesday, July 24, 2013

MCHEZO WA KIRAFIKI BAYERN MUNICH vs FC BARCELONA LEO!Leo usiku saa moja na nusu (19:30) kwa saa za Afrika mashariki, washinda wa kombe la mabingwa barani Ulaya (EUFA Champions League ) Bayern Munich  watakutana kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uhispania FC Barcelona.

Ikumbukwe mechi mbili za mwisho FC Barcelona ilichezea kichapo cha jumla ya magoli 5-1..

Ingawa ni mchezo wa kirafiki utavuta hisia za wapenzi wengi wa soka..

Mpira dakika 90 tusubiri tuone muziki leo..

Tutafika Tu!

Tuesday, July 23, 2013

BREAKING NEWS!! MAMA WA SEGERE -FATUMA RAJABU KAAGA DUNIA LEO (R.I.P)

(Msanii wa kundi la Segere Bi Fatuma Rajabu aliyeshika mkono kichwani)

Msanii wa kundi la SEGERE original Bi Fatuma Rajabu aliyepata kutambana na wimbo wa SEGERE amafariki dunia leo jioni kwa tatizo la upungufu wa damu.


Tutazidi kuwapatia taarifa zaidi kuhusu msiba huu.

Pole kwa familia,wapenzi wa segere na watanzania.


Mwenyezi Mungu aipokee roho ya Fatuma .AMENUnaweza kusikiliza wimbo wake kwa KUBOFYA HAPA

Monday, July 22, 2013

"KODI YA 'SIM CARD' NI KWA AJILI YA KUENEZA UMEME VIJIJINI " Mh Mizengo Pinda (PM)

Waziri mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda

Waziri mkuu Mizengo Pinda amesema tozo iliyopitishwa na Bunge ya sh.1,000 ni kwa matumizi ya simu za mikononi SIYO ya kuwaumiza wananchi bali mapato yake yatakwenda moja kwa moja kusaidia kueneza UMEME vijijini.

Wakati huo huo,,siku tano zilizopita waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo  alisema "Mipango yetu ni kwamba ifikapo mwaka 2014 tayari tutakuwa na umeme wa ziada kiasi cha megawati 500 ambao tutauuza nje ya nchi"

Waziri aliongezea kwa kusema, sehemu watakayo wekea mkazo ni kwenye uchimbaji wa gesi.Ila leo waziri mkuu anasema mkazo kwenye "sim card"
Ukitaka kumsoma zaidi Waziri Muhongo bofya HAPA 

Hapa napata tabu nani wa kumwamini.Kwa nini hizi nguvu zisipelekwe kwenye  kukusanya kodi kwenye sekta za madini, kuondoa misamaa ya kodi,kila kukicha makampuni yana madilisha majina ili kupata misamaha,,,

 

Hii ndio Tanzania...

Tutafika tu