Wednesday, September 24, 2008

MSIBA WA TAIFA..BENDERA NUSU MLINGOTI

Leo bendera zime pepea nusu mlingo katika kuomboleza

Baada ya mwanafunzi Matti Juhani Saari(22) kuwauwa wenzake kumi kwa bastola kisha na yeye kujipiga kichwa na kupoteza maisha yake masaa machache baada ya kufikishwa ktk hospitali ya hapa TAMPERE.

Mauaji yametokea katika shule ya Ufundi ya Kauhajoki (bongo VETA).

SERIKALI imetangaza kuwa leo ni siku ya maombolezo na bendera zote zinapepea nusu mlingoti.

Pia waziri mkuu ametoa tamko kutokana na mauaji haya,itapelekwa hoja bungeni "kuangalia" uwezekano wa kufanyia marekebisho sheria ya kumiliki siraha.

Mwenyezi MUNGU azipumzishe roho za marehemu mahala pema peponi.AMINA

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Pole sana Finland, Pole sana ndugu wafiwa kwa tukio kama hili. Habari zimefika hadi hapa Sweden na vijana wengi wameanza kupata wasiwasi isije ikatokea hapa pia kwani haya mambo huambukizana. Pia haya mambo vijana wengi hucheza hii michezo ya TV pia kompyuta kwa hiyo wanaona kuua si kazi au wanasema wanajaribu. Na mwisho inakuwa kweli. Marehemu wastarehe kwa amani.

Christian Bwaya said...

Nimesikitishwa na habari hizi. Nadhani, kama anavyosema dada Yasinta hapo, sababu inaweza kuwa hiyo. Wazazi mna changamoto na aina ya michezo kwa wanenu. Tekinolojia inashakuwa teke.

Pole kwa wafiwa.

Egidio Ndabagoye said...

NInasikitika kwa mauaji haya,pia nasikitika kwa Bongo haya yataanza kutokea muda si mrefu.Yashindwe na yalageee

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yasinta tumeshapoa ingawa roho bado zina baki juu juu.

Maana mpaka sasa takwimu zinaonyesha wafini milioni 1.6 wanamiliki siraha wakati jumla yao ni watu milioni 2.Sawa na kusema asilimia 13 ya wafini wanamiliki siraha.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Kweli Ndabagoye hii hali inatisha kabisa.

Maana haya yakifika bongo itakuwa hatari zaidi.

Maana viditopile sio vingi mikononi mwa watu ila wanaweza kutumia visu.

Tuombee maadili na amani yawepo kwenye jamii zetu na kukabiliana na huu UTANDAAA WIZI

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Bwaya!!
asante sana kwanza kwa kunitembelea.Pili naungana na wewe kabisa,wazazi na jamii kwa ujumla wanawajibu mkubwa sana wa kusaidia jamii hususani watoto katika malezi yao hasa ukilinganisha na tecknologia tuliyonayo.