Thursday, October 30, 2008

MWANAFUNZI ASHAMBULIA WANNE KWA KISU DARASANI TANZANIA.



Mwanafunzi wa kidato cha tatu shule ya sekondari ya St Peter Kimara,Aron Mbando amewashambulia vibaya kwa kisu wanafunzi wenzake pamoja na mwalimu.



Waliojeruhiwa ni Eva Daza, Siwatu Abdallah, Esther Soter, Anzuruni Anzuruni pamoja na mwalimu Peter Salema. Wanafunzi Eva na Siwatu, walijeruhiwa vibaya kichwani, mgongoni, miguuni na mikononi.


Polisi walifika muda mfupi baada ya tukio na kumkamata mwanafunzi huyo ingawa iliwawia vigumu kutekeleza zoezi hilo kutoka na mwafaunzi huyo kuwa na kisu mkononi.


Nawapa pole walikutwa na tukio hilo ,Mola awaponye haraka.Pia jamii tuanze kujipanda vema na utandawazi.


habari zaidi soma hapa

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Jamani mbona sasa dunia imeharibika au ndo mwisho wa dunia nini

Anonymous said...

my God wat is that Edo??????????? Yasinta ni kweli siku za mwiso zimekaribia kabisa!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yaani hayo ni baadhi ya matokeo ya utandawazi.

Inaoneka watoto wetu wanajifunza mengi kuliko sisi enzi zetu..

Mmomonyoko wa maadili ndio unazidi Yasinta

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Matty ndio safari yenyewe ya maendeleo hiyo..

Tumependa bongo so lazima kukubali pia kuna ua.

ilo ndio ua