Monday, January 19, 2009

GRACE MUGABE AMPIGA MPIGA PICHA.


Bi Grace Mugambe (picha na mpiga picha aliyepigwa Richard Jones)



Mke wa rais wa Zimbambwe juzi alimshambulia kwa kuchapa makofi mpiga picha wa jarida la Sunday Times.


Tukio ilo lilitokea juzi baada ya mke wa Mugabe kumaliza "kula matanuzi" ya juma nzima huku akitumia kila siku paundi £ 2,000 kwa siku .

Kisa cha kumpiga mpiga picha huyo ni kitendo cha kupiga hiyoo picha hapo juu...makubwa!!


Kana kwamba hiyo haitoshi alikuwa kabebelea "lijikoba" maana sio wa bei ndogo siwezi kuuita mkoba ukiwa wenyewe na thamani ya £ 2,000 uliobuniwa na Jimmy Choo Style.

Hayo wakati yanaendelea wazimbabwe wanaendelea kufa kwa njaa na hali mbaya ya kiuchumi.


Habari zaidi bonyeza HAPA


Hivi Afrika kwa stahili hii tutafika kweli?

No comments: