NDUGU NA MARAFIKI,
KWA MASIKITIKO MAKUBWA JUMUIYA YA TAMPERE TUNAWALETEA TAARIFA YA MSIBA WA MTOTO MPENDWA ABIGAIL MARJA KILICHOTOKEA JANA 7.01.2009,TAMPERE UNIVERSITY HOSPITAL(TAYS).MTOTO WA CALISTER KAGALI NA SIMO.
TARATIBU ZA MIPANGO YA MAZISHI BADO ZINAENDELEA.UPATAPO TAARIFA HII MJULISHE MWENZIO.
KWA SASA CALISTER KAGALI NA SIMO WAPO NYUMBANI UNAWEZA KUWASILIANA NAO.
TUTAZIDI KUJULISHANA TARATIBU ZITAKAVYOKUWA ZINAENDELEA.
TUNA TOA POLE KWA JUMUIYA NZIMA KWA MSIBA HUU MZITO AMBAO UMEGUSA HISIA ZETU SOTE NA KUTUTIA SIMANZI ISIVYOELEZEKA WANAJUMIYA.TUNAZIDI KUOMBA MWENYEZI MUNGU AWAPE NGUVU FAMILIA,JAMAA NA MARAFIKI KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA..JINA LA BWANA LIBARIKIWE.
MUNGU AMLAZE MAHALA PEMA PEPONI MPENDWA WETU ABIGAIL.AMINA
NB:-
MAELEZO ZAIDI NA TARATIBU ZA MSIBA ZITAWAJIA BAADAYE.
8 comments:
poleni sana kwa msiba uliowapata.
kazi ya mola haina makosa.
apumzike kwa amani.amini
Poleni sana kwa msiba huo!
siku nyingi sijapita hapa kwako Edo,mzima lakini???
POLENI SANA CALISTA NA SIMO NA MUNGU AWAPE FARAJA, NGUVU NA MOYO WA UVUMILIVU KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
BEST REGARDS,
MAMA ALICE.
Tunamshukuru Mungu kwa yote ..tupo pamoja kwenye sala..
Poleni sana Simo na Calista,aidha kwa wote ambao wanaguswa na msiba huu kwa namna moja ama nyingine
Kubunago tupo pamoja.tuzidi kumuombea mtoto wetu mpendwa Mungu aipumzishe mahala pema peponi.Amina.
sisi wa Tanzania mbona hamtupi taarifa za msiba, mpaka tutafute kwenye mtandao, haya tutaona mwisho wenu
Kay:
Taarifa ilisambazwa kwa watanzania wote waishio Finland, Labda hukupata taarifa kwa wakati kutokana na kukosekana email yako kwa wasambazaji wa Taarifa hii.
Post a Comment