Wednesday, April 29, 2009

LAHTI WAMCHUNGUZA MGONJWA KUHUSU MAFUA YA "MFUGOZI"


Picha ya kitumoto,kitimoto,mdudu,mfugozi,mbuzi katol...,penati,kavu etc

Mgonjwa mmoja ambaye alirejea kutoka Mexico anaendelea na uchunguzi wa afya ili kubaini kama amekumbwa na dhahama la mafua ya nguruwe.

Mgonjwa huyu ambaye anafanyiwa uchunguzi Päijät-Häme Central Hospital .Taarifa ya kuwa amegunguliwa ana ugonjwa huo ama la zitatolewa kati ya siku moja au mbili.

Mpaka sasa mamia ya watu wameshapoteza maisha huko Mexico.Sweeden na Dermarkbado wanaendelea nao kuwachunguza raia wao 10 waliokuwa huko Mexico kucheki kama wapo poa.

Wizara ya mambo ya nje ya Ufini imeshauri kama hakuna ulazima sana ni vema kubatilisha safari za kwenda Mexico.

Mungu tulinde na dhahama hii na uwasaidie watu Mexico na jumuiya ya kimataifa kuweza kupataufumbuzi mapema.

Habari zaidi bofya HAPA


Tutafika tu


4 comments:

Kibunango said...

Ina maana Vappu, hii ipite bila ya Mkuu wa Meza?
Damn..!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

haaaaaa..habari ndio hiyo kibunango safari hii itabidi tule bbq za KLM namaanishaze wings...aaaa aaa

Yasinta Ngonyani said...

Kazi kwelikweli bila kiti moto ukizingatia na sasa ndo wakati wa joto umeanza watu na michomo sasa itakuwaje tena :-(

Bennet said...

Huku Bongo mdudu bado hajapatwa na hayo mafua kwa hiyo week end lazima tukasafishe nyota