Thursday, May 14, 2009

THE NGOMA AFRICA BAND WAACHIA NYIMBO MPYA!!


Kundi la The NGOMA AFRICA BAND

The Ngoma Africa band,bendi ya mziki wa dansi yenye maskani yake nchini Ujerumani,
imeachia hewani vibao vikali !

Wamekuja kwa heshima na adabu kwa kuanza kuwasilimia wakubwa hapa nyumbani! kwa kuanza na wimbo Uliobeba jina la "SALAM ZENU" wimbo ambao unachezeka katika kila hali.

Mtunzi wa nyimbo hizo Ras Makunja aka Bw.Kichwa Ngumu akuacha tabia yake ya kutoa hoja kwa Jamii kwa kupitia wimbo mpya uliobeba jina "Furaha ya maisha iko wapi?" pia akusita kuomba asamehewe kwa aliyoyakosa kwa kupitia wimbo wa "Unisamehe" kitu ambacho kinatakiwa kufanywa na kila mwanadamu anapojiona kuwa kuna kosa la aina yoyote lazima amombe msamaha!

Nyimbo hizo mpya utunzi wake kiongozi wa bendi hiyo Ras makunja ameimba kwa kushirikiana na mpiga solo Christian Bakotessa aka Chris-B.

Nyimbo hizo mpya ni baadhi tu ya nyimbo zikazokuwamo katika Album yao mpya ambayo itafyatuliwa wakati wowote kuanzia sasa.
Tafadhali usikose kusikiliza kwa kubonyeza hapa: www.myspace.com/thengomaafric

Tutafika tu!

15 comments:

Anonymous said...

kaka braza ras makunja vipi?yakhe mbona atutambuani hali,badala yake unaingia kwa gear kubwa ya Salam,
gea hii inaonekana kama vile muungwana kweli! kumbe unatembea na mawe mfukoni! unaweza kuyarusha hata msikitini au kanisani,haya Kaka itabidi tuikubali hiyo heshima unayotupatia

Anonymous said...

hii imekaaje? hawajakuja na adabu?kwanza sio kawaida yao kuingia kwa adabu! mbona baba wa kambo bado anarushiwa madongo katika nyimbo zao

Anonymous said...

hello wazee wa kukaanga mbuyu!naona mnaingia kwa kutisha vipi?
Kaka Bro Ras makunja,sasa hili song la Furaha ya maisha iko wapi?
mbona unalipakua wakati kuna mzozo wa Rotsam Aziz na Mengi kulikoni?
Mie unaponiacha hoi timing zako,mpaka utokee mzozo basi lazima utachomoka na jiwe.
any way tushakuzoea na libeneke lako

Anonymous said...

hi!te te te Vicha wetu kweli mistari ya Dunia ina mambo,nimeikubali,ujumbe mkubwa!kuwa usitende sana wema ukazidi uwezo! wema wako utakuwa sanda yako!
wakuu ujumbe nimeukubali kuwa wema usizidi uwezo

Anonymous said...

sasa ras bwana kichwa ngumu,unanishangaza kidogo hebu niambie unapowapa heshima wakubwa kwa kuwasilimia harafu unadondosha beat kubwa na mawe mazito!hii heshima gani? kama si kuwa bip wakongwe? pamoja na hao hao wakongwe wa sikinde na msondo kuwa wanakulea lakini wakichoshwa na mawe watakupiga konzi

Anonymous said...

huu mdundo wenu vipi?kama vile hauna hakili nzuri

Anonymous said...

Makunja tatizo lako kubwa haupitwi na neno,bila noma utaliungia kibwebwe,si unaona mwenyewe uchozi wako katika huu ubeti wa Furaha ya maisha iko wapi? sasa swali nani? ajibu?

Anonymous said...

Ngoma Afrika hongereni sana hii kazi nzuri,kamatieni hapo hapo.

Anonymous said...

machizi wetu hili sasa gwaride jipya,naona kasi siyo ya kawaida,
mziki moto moto,asei mmekuwa wastarabu kidogo kama vile sio nyinyi.Big Up

Anonymous said...

Ustaadhi bw.Kichwa ngumu vipi? mkuu
mbona unawatishia nyau wa kongwe kwa hizi beat zenu?huu mdundo ktk wimbo wa furaha ya maisha iko wapi? ni mziki mkubwa wa kiutu uzima,labda unawa bip wakongwe,subiri wakujibu sasa

Anonymous said...

wazee hili dongo mliorusha mara nzito Fura ya Maisha? mungu wangu sasa nani atoe jibu ? labda mjibu wenyewe.

Anonymous said...

nawakubali kweli nyinyi ni mzimu,
aka ffu aka watoto wa mbwa mwitu kila sehemu mnabwaka.
Kazeni Buti

EDWIN NDAKI (EDO) said...

hakika hawa waheshimiwa waliacha gumzo kubwa sana majira ya baridi hapa ufini.

ni imani yangu watarudi tena..

tutafika tu

Anonymous said...

wazee wa kukaanga mbuyu naona mambo mswano kabisa,leteni raha tunawakubali kuwa no mzimu wa mziki.

Anonymous said...

vichaa wa ngoma afrika hapa mmefunga kazi! kweli nyinyi mbwa mwitu wakali