Wachezaji Kilimanjaro Fc kutoka sweden wakiserebuka baada yakuwabamiza bila huruma timu ya mpira ya wabongo yenye maskani yake jijini Helsinki kwa mabao 8 kwa kamoja.
Kwisha stori:wapo hoi wamekata tamaa mpira umekwisha wameshapewa bilauli 8 za maji.Msijali mpira unadunda.(Picha zote kutoka kwa mdau George Matovu-Mtv)
Kilimanjaro Fc kutoka sweden imeendeleza ubabe kwa kuibanjua Bongo Fc nyumbani kwao Heslinki magori 8-1.
Bongo Fc walionekana kuzidiwa kimchezo,mpaka kipindi cha kwanza kinaisha Kilimanjaro FC walikuwa wanaongoza kwa magoli 5 kwa nunge.Kipindi cha pili Bongo Fc walifanikiwa kujipatia kagoli kakufutia macho.
Mpaka mwisho wa mtanange,Kili Fc 8 na ndugu zao Bongo Fc 1.
Kilimanjaro Fc wameibugiza bongo fc magoli 8-1
Ikumbukwe mara ya mwisho walikutana mwaka jana Sweden na Kilimanjaro kuibuka washindi 4-3.
Pongezi sana Kilimanjaro Fc kwa ushindi mnene.Poleni sana majirani Bongo Fc kwa kichapo cha mwaka...aaa aa
Tutafika tu
5 comments:
Haha haahaahahahahahahaha nashindwa kuacha kucheka kwa kweli hehehehehehehehe KAMOJA tuuuuuuu ka kunywea maji au siooo
tulikuwa tumetingwa na shule,hatukufanya mazoezi. subirini game jingine muone kilichomtoa kanga manyoya!
bongo fc walikuwa wanategemea wakenya..baada yawakenya kuanzisha timu yao ndio ilikuwa mwisho wa stori.itabdi warushwe tena bongo fc
pole edo... sasa we leo ulikuwa kipa au ulicheza ndani..inaonekana ulikuwa umekunywa maji ya ugwadu nini..aaa
mhm hiki kipigo noma, kinanikumbushe vile vipigo vya 7-3 na 7-4 walivopewa Tampere na jamaa wa Helsinki hapo mwaka 2007. Na hio 5-0 mpaka halftime si alifanyiwa Tampere kwake mwaka 2008 ;-)
Post a Comment