Monday, June 15, 2009

MGOMO NCHI NZIMA USAFIRI WA 'TRAIN'

Magari moshi yakiwa yamezimwa kwa ajili ya mapumziko ya mgomo
Ubao wa matangazo ukiwa "mweupee" bila taarifa yoyote
Sehemu ambayo mara nyingi inakuwa na wasafiri leo ilikuwa haina mtu.
Ofisi za kukatia tiketi nazo nilikuta zimefungwa.


Leo wafanyakazi wa shirika la reli hapo Ufini wameamua kufanya mgomo wa siku zima.Mgomo huo wa nchi nzima umeitishwa katika madai yao ya kurekebishwa "maslai ya kazi".

Mgomo huo wa siku moja utaisha leo usiku na kuanzia kesho alfajiri saa tisa usafiri utakuwa kama kawa.Ila jamaa wamesema wakiona serikali haijafanyia kazi madai yao basi wanapanga kufanya mkubwa zaidi.

Duh! ..

Ni hayo tu kwa leo...kumbe hata maulaya ulaya bado vilio tu kama zebongozi?

Tutafika tu

4 comments:

Yasinta Ngonyani said...

kaka Edo kazi kwelikweli!!!!

Unknown said...

yaani si kidogo ndugu yangu

PASSION4FASHION.TZ said...

Oh! kaka Edo nilipita kusalimia,bahati mbaya nimekumbana na huu mgomo,sasa sijui ntarudije kijiweni kwangu? hahahahaaaa!!!! karibu saaana!!!

Anonymous said...

Edo, Hawa jamaa nasikia mgomo wao sio kudai maslahi peke yake, lakini pia wamechukizwa na tabia ya serikali yao kuanza kubadilika kwa kufikiria biashara(faida) zaidi kuliko ubora na usalama wa abiria. Wanawalinda wananchi wenzao!