Baada ya kuwafunga Congo aka watoto wa Kabila dada zetu waliongoza jahazi la ukarimu kwa kuwapatie sombe na mnuso wa nguvu.
Leo "wamefulia" wachezaji wa DR Congo wakijikusanya kabla ya mpambano kuomba mvua inyeshe lakini matokeo yake jua likawaka
Shabiki namba moja wa timu ya Kongo akiwa na bendera ya nchi yake.Ila baada ya kufungwa sikuiona TENA hiyo bendera.
Kikosi cha timu ya Tampere Africans Sports(TAS) kabla ya mpambano dhidi ya Kongo.Huyu aliyechuchumaa kutoka kulia ni kocha viuongo kutoka 'Brazili'..aaa mwaka huu
Kocha mkuu wa timu ya TAS George Matovu ukipenda muite MTV akiweka mikakati ya ushindi.Salaam kwa bongo FC na Kilimanjaro stars.
Timu ya Tampere Africans Sports (TAS) inayoundwa na wabongo imefanikiwa kuibanjua bila huruma timu ya kutoka jiji la Helsinki inayoundwa na wachezaji kutoka jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Tas imeondoka kifua mbele kwa kuifunga magoli 4-1 Congo.Baada ya mchezo wachezaji na watazamaji walishiriki mnuso wa pamoja ukiambatana na viburudisho na buradani za hapa na pale.
Wakati huo huo
Timu ya wabongo ya BONGO FC leo imeshuka dimbani kupambana na timu ya Wacameroon ila mpaka muda huu mpambano unaendelea tutawaletea matokeo.
Hongera TAS kwa ushindi mnene!!
Tutafika tu
1 comment:
Utaratibu umekaa vipi kwa wale walioshindwa kuhudhuria mtanange huu, hasa katika maeneo ya makulaji?...:D
Post a Comment