Moja ya nguzo yenye taa za kumwaga ukidondosha hata sindano usiku utaiona
Leo mchana nimefika mapema kupata ppicha mbili tatu kabla ya mtanange kuanza.
Uwanja ulikuwa umechemka naona jamaa wanaupoza maana leo itakuwa game kali
Maafisa wa EUFA wakikagua uwanja wa Ratina hapa jijini Tampere kabla ya mpambano wa timu ya taifa ya wanawake ya Ujerumani na Ufaransa
Nipo uwanja wa mpira wa miguu wa jiji la Tampere Ratina kusuburia mpambano wa ligi ya mabingwa barani ulaya wanawake UEFA WOMEN'S EURO 2009
Ujerumani walicheza mechi yao ya kwanza na kuwabanjua 4-0 Norway huku Ufaransa wakilamba dume kwa kuwafunga 3-1 Icelanda.
Sasa leo wanakutana wababe hao wawili kuoneshana nani zaidi.
Nitawaletea picha habari baada ya game.
Tutafika tu
No comments:
Post a Comment