Thursday, December 31, 2009
GIVE THANKS TO GOD
Kwanza natumia nafasi hii kuwaomba msamaha wale niliowakwaza kwa kushindwa kuweka mitundiko kwa siku kadhaa,hiyo ilitokana na purukushani za maisha.SASA nimerudi.
Leo naomba tukumbushane KUSHUKURU.
Wangapi tulioanza nao mwaka huu hatunao?
Kuna watu mwaka huu huu wamepoteza wapendwa wao,hakika ni uzuni.
Wengine wako magereza wamefungwa kwa kuonewa.
Wengine wapo mahututi hospitalini au wamepata ulemavu kutokana na ajali.
Hivyo tuna kila SABABU ya KUMSHUKURU Mungu kutujalia uzima mpaka siku ya leo.
Kama mwaka 2009 ulikuwa mgumu basi usikate tamaa,weka mikakati "God is able" mambo 2010 yatakuwa POA.
Binafsi namshukuru Mungu kuniwezesha kuweka mtundika siku hii ya leo.Nawashukuru pia wazalendo woote kwa kunitembelea bila kuchoka.
Nawatakia afaya njema tuweze kumaliza salama 2009.
Inshallah Mungu akipenda tutaonana 2010.
Siku njema
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment