Wednesday, February 24, 2010

MKENYA MBARONI KWA KUSAMBAMZAZI HIV KWA MAKUSUDI

Picha zikimwonyesh Judith Osmondi -Mäkelän aka Rachel anayetuhumiwa kusambaza hiv /aids.
Kwa siku mbili mfululizo vyombo vya habari habari,mitandao imakuwa ikichapisha habari za dada raia wa Kenya ambaye amekiri kufanya mapenzi yasiyo salama na watu mbalimbali ili hali akijua kuwa ana VVU/Ukimwi tangu mwaka 2005 hadi leo.
Rachel kama anavyoonekana kwenye moja ya gazeti la "udaku" la hapa.Rachel alitoa idhini pia kwa polisi kuchapisha picha yake ili itumike kukusanyia ushahidi kwa kuwaomba watu waliofanya naye mapenzi wakapime na kupeleka taarifa zao polisi.(picha na habari kutoka www.iltasanomati.fi
Raia wa Kenya Judith Osmondi amefikishwa katika mahakama ya jiji la hapa Tampere kwa tuhuma za kusambaza VVU/ukimwi kwa makusudi huku akijua kuwa ana maradhi hayo. Hiyo ni kwa mujibu wa taarifa alizotoa muhusika.

5 comments:

chib said...

Kwa kweli angekuwa mitaa ya Manzese hivi, nafikiri hazina ya mawe yote yaliyopo yangemuonja.

Kitendo hicho ni kibaya sana na wala hakifai kabisa

John Mwaipopo said...

really bad! hana hata chembe ya huruma.

Anonymous said...

Anastahili kifo!!

Habari said...

Huyo Mkenya ametuaibisha sana watu wa Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla.Yaani watu wanatafuta maisha yeye anangonoka tu matokeo yake ndiyo hayo kuwaambikiza wengine kwa makusudi.

From Benjamin Sawe

Information Officer

Ministry of Information Culture and Sports

Unknown said...

Hivi jamani mtu unakuwa na roho nguvu kiasi gani kufanya kitu kama hicho, istoshe anafanya waafrika wengine wote waliohuko Finland kuonekana hivyo hivyo tuu. Kwakweli huyu dada anastahili kifo ukizingatia ameshachongeshea kaburi kwa hao wengine..Hana haya kabisa,,yaani miaka 5 kusambaza kitu kama hicho..dah imenigusa sana, swali langu...is it ok kuitumia hii kwenye kibaraza changu?/naxy