Monday, June 14, 2010

Mchungaji kutoka Rwanda maisha jela kwa mauaji



Pastor Francois Bazaramba

Pastor Francois Bazaramba akiwa mahakamani akisikiliza kesi yake.
(Picha kutoka hs.fi na Jussi Nukari)

Raia wa Rwanda aliyekimbilia hapa Finland(Ufini) mwaka 2003.
Amehukumiwa na mahakama ya mji wa Porvo0 hapa Finland baada ya kukutwa na hatia ya kuhusika katika kushiriki kwa mauji ya kimbali yaliyotokea nchi rwanda na kupelekea vifo vya zaidi ya watu 800,000 mwa 1994

Mchungaji Bazaramba amekuwa akishikiliwa tangu mwaka 2007 hadi hapo juzi hukumu yake ilipotolewa.Mahakama imetumia takribani euro milioni moja katika kusikiliza kesi yake,hii ikijumuisha gharama mbalimbali moja wapo ilibidi watendakazi wa mahakama ya finland kwenda rwanda na Tanzania kukusanya ushahidi zaidi.

Hii imekuwa kesi ya kwanza kwa ukanda wa nchi za "scandinavia" kusikiliza kesi ya namna hii.Rwanda iliomba mtuhumiwa arudishwe nchini kwake ili kesi yake isikilizwe kama watuhumiwa wengine,lakini serikali ya Ufini ilikataa kwa madai mtuhumiwa anaweza asitendewe haki.

Habari zaidi isome kwa KIINGILISH gonga HAPA

Tutafika tu

No comments: