Thursday, December 29, 2011

BI HALIMA MCHUKA HATUNAYE TENA - R.I.P

Bi Halima Mchuka enzi za uhai wake.

Leo nimepokea habari ya kustusha baada ya kutembelea ukurasa wa Facebook wa mmoja wa marafiki zangu na kukutana na picha na habari mtangazaji mkongwe Bi Halima Mchuka hatunaye tena kaaga Dunia.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa TBC Clement Mshana, Bi HALIMA MCHUKA alikimbizwa katika hospitali ya DAR GROUP na baadae katika hospitali ya Taifa ya MUHIMBILI hapo jana baada ya kuanguka ghafla akiwa katika kituo chake cha kazi eneo la PUGU ROAD Jijini DSM.

Binafsi nilibahatika mara kadhaa miaka hiyo kumsikiliza akitangaza mpira wa miguu.Hakika alijaaliwa kipaji na alikuwa na mapenzi na soka.Bi Halima Mchuka atakumbukwa kwa historia aliyojiwekea ya kuwa mtangazaji wa kwanza mwanamke wa soka katika ukanda wetu wa afarika ya mashariki.

Mwenyezi ailaze roho ya Bi Halima Mchuka mahala pema peponi .Amina

No comments: