Monday, October 29, 2012

HONGERA MDAU DR Ayub Rioba UMEKULA NONDO YA UDAKTARI WA FALSAFA (PhD).




Naam! sasa utaitwa Dr Ayub Rioba, muda mfupi baada ya kutunukiwa sahada ya udaktari wa Falsasa(PhD) katika  Sayansi ya Jamii, Chuo kikuu cha Tampere katika jiji la Tampere, Finland.


Meza kuu kutoka kushoto Dr Ayub Rioba (University of Dar es salaam, Tanzania) Prof Kaarle Nordenstreng (University of Tampere, Finland) pamoja na Prof Audrey Gadzekpo (Accra University, Ghana).DR Rioba akijibu moja ya maswali kutokana na utafiti wake wa  "Media accountability in Tanzania's Multiparty democracy: Does self regulation work?"




Kutoka kushoto Prof Kaarle Nordenstreng, University of Tampere Finland  pamoja na Prof Audrey Gadzekpo akiongoza mchakato wa kumtunukia falsafa ya udakati Ayub Rioba.

Blogger  Edo Ndaki akiwa pamoja na Khalifa Mjengwa muda mfupi baada ya Dr Ayub Rioba kulamba nondo .
(Picha zote na Paula Paukku - University of Tampere,Finland)

Leo katika Chuo Kikuu cha Tampere, jijini Tampere,Finland, mdau Ayub Rioba amekula nondo shahada ya udaktari wa falsafa(PhD) katika sayansi ya jamii.

Kabla ya kula nondo yake alitumia zaidi ya masaa mawili kutetea tafiti yake ya "Media accountability in Tanzania's Multiparty democracy:Does self regulation work?"

Baada ya mjadala mzito wa kitaaluma na maswali kibao ya Prof Audrey Gadzekpo kutoka Chuo kikuu cha Accra, Ghana pamoja jopo la maprofessa walifikia hitimisha na kumtunukia shahada ya Falsafa ya Udakati(PhD) katika fani ya Sayansi ya jamii.

Wadau wanakupongeza kwa hatua hiyo ,na kukutakia kila kheri katika kuitumikia jamii..
Hongera DR AYUB RIOBA!

Tutafika tu


2 comments:

Boneka Full Body said...

good sharing and information

Vimax Asli said...

nice blog and article