Habari za hivi punde tu.Mwanafunzi anaye kadiriwa kuwa na umri wa miaka 20 amevamia Chuo chake cha ufundi na kuua wanafunzi tisa ,kujeruhi vibaya wawili na wengine wakiachwa majeruhi.Muuaji huyo alijipiga pia risasi ingawa bado yupo hai.
Mwaka jana mwanafunzi mwanafunzi Pekka-Eric Auvinen(18) alivamia shule kwao na kuua wanafunzi na wafanyakazi nane.
Sheria za hapa Ufini mtu mwenye umri kuanzia miaka 15 anaruhusiwa kumiliki siraha.Kitu kinachopelekea nchi ya FINLAND kuwa ya tatu duniani kwa wananchi wake kumiliki siraha huku USA na Yemen zikiongoza.
Binafsi natoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao.Najua ni kipindi kigumu kwao.
Naomba mwenyezi Mungu awape moyo wa ujasiri na uvumilivu.
Roho za marehemu wapumzike kwa Amani.Amina
Habari zaidi soma BBC