Tutafika tu
Blog
Thursday, June 11, 2020
Friday, February 24, 2017
YAMOTO BAND EUROPEAN TOUR - FRANKURT GERMANY ( JMOSI FEB 25,2017)
YAMOTO BAND JUMAMOSI 25/02/2017 JIJI LA FRANKFURT UJERUMANI.
Yamoto Band tangu kuwasili mwanzoni mwa February wakiwa wameambatana na meneja wa Chambusso , wamafanya maonyesho Stockholm -Sweden, Wegackerstrasse Leimbach -Switxerland, Oslo-Norway, Helsinki -Finland, Copenhagen - Denmark and Frankfurt Germany.
Mbali na maonyesho, Yamoto Band wameshiriki kwenye madarasa mbalimbali kufundisha (workshop) sanaa ya kitanzania na pia kupata fursa ya kujifunza na kurekodi kazi zao mpya kwenye studio za kisasa hapa Finland.
Wadau wa Ujerumani mjitokeze kwa wingi kwenye shughuli ya JUMAMOSI FEBRUARI 25, 2017 Frankfurt.
Friday, February 17, 2017
TAARIFA YA MSIBA STOCKHOM SWEDEN: BW SALVATORY RUTAHINDUKA KAMALI (R.I.P)
Marehemu Bw Salvatory Rutahinduka Kamali (RIP)
Jumuiya ya watanzania Sweden, inasikitika kutangaza kifo cha ndugu yetu mpendwa SALVATORY RUTAHINDUKA KAMALI
kilichotoea February 16, 2017 kwa kuangukiwa na gari akiwa kazini Sweden.
Kwa sasa mwili wa marehemu umeifadhiwa hospitali kwa uchunguzi, mara polisi watapokamilisha taratibu zao mtajulishwa taratibu za wapi kukutana na jinsi kuchangisha rambirambi kwa ajii ya kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa mazishi.
Marehemu hana ndugu aliyepatikana hapa Sweden hivyo kwa maelezo zaidi unaweza wasiliana na
+ 46 70-642 43 99 SKOLA
+ 46729265552 NORMAN
+ 46729265552 NORMAN
TAFADHALI SAMBAZA UJUMBE HUU KWA WENGINE NI MSIBA WETU NA MARAFIKI ZETU.
Pumzika kwa amani. Amina
Leo nairejesha EDONDAKI.BLOGSPOT.COM baada ya mapumzika ya miaka miwili na nusu..NIPOKEENI
Pichani jana nikiwa mji mkuu wa Jamuhuri ya Czech, Prague.
Salaam kutoka Jamuhuri ya watu wa Czech. Nilianza kublog mwaka 2007 hadi 2014. Baadaye niliamua kupumzika kublog. Nilipendelea kutuma picha na habari fupi, ikiwa ni sehemu ya kutumia taaluma yangu ya habari niliyoipata chuo kikuu cha SAUT mwanza na Tampere,hapa Finland.
Baada ya mapumziko ya tangu Juni 2014, ikiwa ni miaka miwili na miezi saba, leo nimeamua kurejea kwenye hili 'libeneke' kama anavyoliita nguli wa blog ISSA MICHUZI .
Mengi yamejitokeza, blog nyingi zimezaliwa na kufa ktk kipindi hiki. Sisi tulipoanza ilikuwa lengo kuu ni kuhabarisha, kabla kuwa 'chanzo cha kipato'.
SASA NAREJEA TENA KWENYE HII MEDANI. TUTAFIKA TU
Kama ulivyo msemo mkuu wa hii blog TUTAFIKA TU.
Wasalaam
Edo Ndaki
edondaki.blogspot.com
Prague, Czech.
17-02-2017
Monday, June 23, 2014
BONGO FC (Finland) WAISAMBARATISHA NIGERIA 4- 2
Timu ya watanzania Bongo FC yenye maskani yake Finland.Picha baada ya pambano lake na timu ya Nigeria na kufanikiwa kuzoa ushindi mnene wa mabao 4-2.
Bongo FC miongoni mwa timu kongwe na kielelezo cha uwakilisha wa Tanzania kwenye ukanda wa nchi za 'scandnavia'.
Bongo FC imefanikiwa kuanza kampeni yake ya msimu wa majira ya kiangazi kwa kucheza michezo miwili.Mchezo wa kwanza waliifunga timu Ethiopia magoli 5-3 na mwishoni mwa juma kuifunga timu ya Nigeria 4-2.
Wafungaji wa magoli akiwa Mwita Chacha , Bakari Salehe, Tonny aka Diego Simeon..Hizi ni salaam kwa ndugu zetu wa Sweden Kilimanjaro FC...
Hongera Bongo FC

Friday, May 30, 2014
WORLD VILLAGE FESTIVAL 2014-HELSINKI FINLAND
Baadhi ya watanzania waishi jiji la Helsinki Finland picha ya pamoja muda mfupi baada ya maandalizi ya banda la jumuiya ya watanzania na finland (STS) kwenye maonyesho ya "World Village Festival'
Kutoka kulia Noeli Makumuli mjumbe wa bodi , msaani wa kimaitaifa wa Raggae kutoka Tanzania Jhikoman pamoja na Edo Ndaki Mwenyekiti wa Finland Tanzania Friendship society - STS
Picha huongea maneno zaidi ya elfu moja.Hakika banda la wawakilishi wa Tanzania lilifana na kutembelewa na wageni wengi.
Kutoka kulia bw Fidelis Tungaraza akitoa ufafanuzi kwa mgeni aliyetembelea banda huku bw Edward Mtafungwa na Noel Makumuli viongozi wa bodi ya STS wakiendelea kuhabarisha wageni mambo mbalimbali yahusuyo Tanzania.
Mark Mhekwa kati ya watanzania waliopata muda wa kutembelea banda la maonyesho la jumuiya ya watanzania na wafini.
Naam,Moudy alimletea binti yake kumnunulia vitabu pamoja na cd za kiswahili ili aweze kujifunza lugha ya baba.Safi sana.
"One loveeeeeeeeeee" kutoka kushoto msanii wa muziki wa Raggae kutoka Bagamoyo Tanzania Jhikoman, nguli Popo pamoja na makamu mwenyekiti wa jumuiya Ilona Tika.
'Karibu Tanzania' nilitembelea na mwanafunzi ninayesoma naye chuo kimoja .Hakuondoka hivi hivi alivutiwa na kitabu chetu cha 'KARIBU TANZANIA'
Wadau wa jiji la Helsinki..Hii picha naomba msaada wa caption :D
Kutoka kulia Noeli Makumuli mjumbe wa bodi , msaani wa kimaitaifa wa Raggae kutoka Tanzania Jhikoman pamoja na Edo Ndaki Mwenyekiti wa Finland Tanzania Friendship society - STS
Kutoka kulia bw Fidelis Tungaraza akitoa ufafanuzi kwa mgeni aliyetembelea banda huku bw Edward Mtafungwa na Noel Makumuli viongozi wa bodi ya STS wakiendelea kuhabarisha wageni mambo mbalimbali yahusuyo Tanzania.
Mark Mhekwa kati ya watanzania waliopata muda wa kutembelea banda la maonyesho la jumuiya ya watanzania na wafini.
Wadau wa jiji la Helsinki..Hii picha naomba msaada wa caption :D
Sunday, March 30, 2014
TUTAFIKA TU: NAAM!! NIMEPATA NGUVU YA KUREJEA KUBLOG TENA!
Edo Ndaki pichani nikiwa kwenye moja za 'SAFARI' za hapa napale jiji, Tampere Finland.
Habari za tangu mwaka jana 2013.Hakika nilihadima kwenye medani ya 'kublog'. Majukumu ya hapa na pale yalinifanya nikose fursa ya kuwasiliana na blog wenzangu na hata wasomaji wangu.
Nafarijika kila kukicha nionapo 'indastri' hii inavyukua. Nawapongeza marafiki ambao kwa miaka nenda rudi wamekuwa na nguvu ya kuendeleza libeneke kwa miaka kadhaa sasa. Hakika tambueni chango wenu ni mkubwa,endeleeni bila kuchoka.
Kama ilivyokauli kauli mbiu ya blog hii "TUTAFIKA TU" basi naamini tutafika tu.Nitaendelea kuwaletea matukio mengi zaidi yanayotokea huku niliko Ufini pamoja na majirani zangu huku barani Ulaya yenye manufaa kwa wadau wote.
Asante kwa kunisoma.
TUTAFIKA TU.

Wednesday, July 24, 2013
MCHEZO WA KIRAFIKI BAYERN MUNICH vs FC BARCELONA LEO!
Leo usiku saa moja na nusu (19:30) kwa saa za Afrika mashariki, washinda wa kombe la mabingwa barani Ulaya (EUFA Champions League ) Bayern Munich watakutana kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya mabingwa wa Uhispania FC Barcelona.
Ikumbukwe mechi mbili za mwisho FC Barcelona ilichezea kichapo cha jumla ya magoli 5-1..
Ingawa ni mchezo wa kirafiki utavuta hisia za wapenzi wengi wa soka..
Mpira dakika 90 tusubiri tuone muziki leo..
Tutafika Tu!
Subscribe to:
Posts (Atom)