Jumapili april 22,2012 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein,ameongoza maelfu ya wananchi na viongozi mbali mbali wa Serikali katika mazishi ya aliyekuwa Brigedia Jenerali Msataafu Marehemu Adam Clement Mwakanjuki ambayo yamefanyika Makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar.
Mazishi hayo ambayo yalifanyika kwa heshima zote za kijeshi kwa kupigwa mizinginga 11 baridi, yalihudhuriwa pia na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzani Dk.Gharib Bilal,Rais Msaafu wa Zanzibar Aman Abeid Karume,na viongozi wengine wa ngazi za juu wa Vyama vya siasa na Serikali.
Chanzo:Asante Othuman Mapara kwa picha
Blog hii inawapa pole familia kwa msiba huu.Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.Pumzika kwa amani Brigedia Generali Adam Mwakanjuki.Amen
Chanzo:Asante Othuman Mapara kwa picha
Blog hii inawapa pole familia kwa msiba huu.Mwenyezi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu.Pumzika kwa amani Brigedia Generali Adam Mwakanjuki.Amen
No comments:
Post a Comment