Sunday, July 22, 2012

East African Team(Tampere) yaipiga STOP!! Bongo Fc(Helsinki)

 Timu ya mpira wa miguu East African Team  inayomilikiwa na East African Sports and Culture Ry yenye makazi yake jiji tampere,Finland wakiwa kwenye picha ya pamoja.

Mshambuliaji wa timu ya East African Team Fanny Abdul akiunganisha pande juu kwa kutoka kwa Zakaria Masoud (huyupo pichani) na kuandika bao la tatu.

Dakika 83 kabla ya mchezo kuisha  Zakaria Masoud(East African Team) akiweka kimyani bao kwa mkwaju wa penati kufuatiwa kuchezewa madhabi  na mlinzi wa timu ya Bongo FC.
Mlinda mlango wa timu ya East African Edo Ndaki(kulia mwenye magongo) ambaye kwa sasa anauguza jeraha lakuteguka goti akiwa sambamba na mkurugenzi wa Extra Bongo Band kamarade Ally Choki muda mfupi baada ya mpambano kati ya East Africa Team ya Tampere City  dhidi ya watani wao wa jadi Bongo Fc kutoka jiji la Helsinki.(picha Zote na L.Karlin)

BONGO FC yalazimishwa suruhu ya mabo 4-4 dhidi ya timu changa ya East Africa a.k.a "Uamsho" iliyoundwa miezi miwili iliyopita.

Bongo Fc ilitua jiji Tampere wakiwa na kikosi kamili tayari kuonyesha makucha yake baada ya kuchezea vichapo mechi mbili mfululizo kwenye mashindo yanayoshirikisha timu za kutoka mataifa mbalimbali jiji helsinki,Finland

Bongo Fc ndio walikuwa wakwanza kucheza na nyavu na kuandika mabao 2 ya haraka  na kupelekea mpaka kipindi cha mapumziko East Africa 0-Bongo Fc 2.
Kipindi cha pili kilianza kwa vuta nikuvute na East Africa walifanikiwa kusawazisha.Zikiwa zimebakia dakika 20 Bongo Fc kupitia mshambuliaji wa John aka Mafe Lingz aliweza kuipatia timu yake bao ya 3.

East African wakionyesha kujiamini na kumiliki mpira kwa asilimia kubwa kupitia mshambuliaji wake wa pembeni Zakaria Masoud alipiga pande zuri lililounganishwa juu kwa juu na Fanny Abdul na kuandika bao  3-3.

Dakika 83 Zakaria Masoud alitia kimyani bao la kuongoza kwa njia ya penati ya kuwaacha mshabiki wa Bongo Fc wamechanganyikiwa.

Mwamuzi wa mchezo huo Mzee Mataluma aliweza kuhumuda vema mchezo kwa kipindi chote cha Dakika tisini.
Mpira dakika 90..Bongo Fc walifanikiwa kusawazisha katika dakika za nyongeza,mpaka mwisho wa mchezo East African Team 4- 4 Bongo Fc.

Baada ya mchezo timu zote mbili zilijumuika kwa chakula cha jioni na baadaye kuelekea katika tamasha la FEST AFRIKA ambako Awilo Longomba alikuwa akitarajiwa kupanda jukwaani.

Mechi ya marudiano inatarajiwa kuchezwa July 28,2012 katika mji wa Helsinki.

Tutafika tu


1 comment:

Celana Hernia said...

I visited several web pages however the audio quality
for audio songs existing at this website is truly fabulous.