Tuesday, July 24, 2012

NAMSHUKURU MUNGU NAENDELEA VEMA

Edo pamoja na Roggat Hegga muimbaji wa Extra Bongo Band

Namshukuru Mwenye Mungu kwa sasa naendelea vema na jeraha langu la goti nililopata wakati wa mchezo wa kirafiki kati ya timu yangu ya Tampere ilipocheza na timu jirani kutoka mji wa Vaasa.

Mbali na kuumia ujio wa Extra Bongo Band ulikuwa faraja na tiba mbadala katika kipindi hiki.
Naam kwa sasa wanaelekea jijini Helsinki kwa ajili ya onyesho la mwisho  kabla ya mwisho wa juma hili kuekelea Stockholm Sweeden na nchi nyingine barani Ulaya.

Nawatakia kila kheri katik ziara yenu,iwe na mafanikio zaidi.

Wasalaam Edo

Tutafika tu!

2 comments:

Yasinta Ngonyani said...

pole sana kaka Edo. Ugua pole utapona tu...ila usisahau kufanya fanya mazoezi...

Obat Vimax said...

yes i like it this blog and article. thanks