Wednesday, August 22, 2012

Ngoma Africa Band KUVAMIA Alafia Festival, Hamburg


Chris B(kushoto) mdau na Kiongozi wa Ngoma Africa Band aka FFU  Ras Makunja wakiwa na tuzo zao.
Bendi maarufu ya muziki wa dansi barani ulaya "Ngoma Africa Band" aka FFU
watatingisha jukwaa la ALAFIA Festival,mjini Hamburg,Ujerumani siku ya
jumapili 26.8.2012 .

Onyesho hilo kubwa la wazi linafanyika mji wa Hamburg, eneo la maarufu la  Hamburg-Altona

Ngoma Africa band imetajwa moja ya bendi bora katika maonyesho mengi ya kimataifa na kupelekea kushinda tuzo ya kimataifa ya" IDA-International Diaspora Award".Kikosi kazi hicho kinachoongozwa na mwanamuziki Ebrahim Makunja aka kamanda

Mtanzania Ras Makunja ndiye anayeongoza kikosi kizima cha Ngoma Afrika aka FFU akishirikiana na makamanda wengine akiwem kamanda wake Christian Batokess aka Chriss B
Kwa sasa Ngoma Africa Band wanatamba na CD mpya "Bongo Tambarare" ambayo unaweza kuisikiliza kupitia tovuti yao ya www.ngoma-africa.com

Kwa niaba ya wasomaji wa blog hii tunawapongeza FFU  kwa kuchukua tuzo endelezeni gwaride.
Tutafika tu.

1 comment:

Anonymous said...

hongereni sana FFU wazee wa gwaride kubwa,aka watoto wa mbwa,mnakubalika kimataifa.