Wednesday, July 25, 2012

NDANI YA DAKIKA CHACHE TIKETI ZA ONYESHO LA JUSTINE BIEBER ZANUNULIWA ZOTE "SOLD OUT"-FINLAND

 Msanii wa pop Justine Bieber pichani alipotwaa moja ya tuzo.
Msanii Justine Bieber akiwa na meneja wake Scooter Braun .Scooter alikutana na video ya Bieber kwenye mtandao na kuamua kumtafuta na kumsaidia kimuziku.Ni mtu muhimu sana kwenye mafanikio ya "game yake".


Msanii wa muziki wa pop Justine Drew Bieber aliyezaliwa  machi 1,1994 Stratford  Ontario Canadian atafanya onyesho lake April 2013  kwenye jiji la  Helsinki Finland.
Kwa mujibu wa waandaaji wa onyesho Fullsteam  jana july 24,2012 mauzo ya tiketi yalipofunguliwa rasmi ndani ya dakika chache tiketi zote zilinunuliwa na wapenzi na mashabiki wa Justine Bieber.Tiketi iliyokuwa ya gharama ndogo ni 75euro(sawa na takribani shilingi 140,000/= pesa ya tanzania)
Watu 12,000 wanatarajiwa kuhudhuria onyesho ilo katika eneo la Helsinki Arena ilikuweza kumuona msanii huyo ambaye atakuwa kwenye ziara yake aliyoipa jina "Believe Tour" .
Scooter Braun alitambua kipaji cha Bieber baada ya kukuta video yake kwenye mtandao wa youtube  na baadaye kuwa meneja wake na kuunganisha na msanii Usher Raymond na baadaye mtayarisha wa muziki LA Reid.
Bieber kwa mwaka 2012 ametajwa na jarida la Forbes kushika nafasi ya tatu ya mastaa ambao wako juu kwa sasan na ameweza kujiingizia kipato za zaidi ya  USD 55milioni kwa miezi 12 iliyopita na kuuza zaidi ya rekodi milioni 20,na ni miongoni mwa wasanii wenye wafuasi wengi mtandao wa kijamii wa twitter akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 25
"Boyfriend" ndio wimbo wake mpya ambao umeshika nafasi za juu kwenye nchi zaidi ya 30 duniani.
Chanzo:mitandao ya habari
Tutafika tu