Saturday, July 12, 2008

SAFARI YA MUUJIZA KWENDA ULAYA!!



Mtoto Daniel Masinde(16)akiwa nje ya uwanja wa Ndege Dsm.Akiwa pamoja na waumini wenzake wa kanisa la Wasabato masalia,wakisubiri safari ya kuelekea Ulaya kuhubiri injili.

Wapo hapo wakisubiri kusafiri kwa miujiza ya bwana Yesu bila pasi za kusafiri wa visa wala tiketi.Kwa madai yao Bwana yesu ndio atatoa visa,tiketi na kila kitu.Na huko waendake watajazwa roho mtakatifi wataongea lugha yoyote.

Mtoto Daniel alikuwa kafaulu kuendelea na masomo ya sekondari huko Mkoani Mara,lakini mtoto huyo akanona bora kwanza aubiri injili shule itafuate baadaye.

Duh..hii imekaaje ..tutafika kweli?

http://mwananchi.co.tz/newsre.asp?id=5914

7 comments:

Anonymous said...

hivi hawa watu wako serious kweli???? au ????maana inawezekana wapo serious lakini hawajawezeshwa sasa hapo napo ni tabu kidogo.
tutafika kweli EDO??

Simon Kitururu said...

Kazi Ipo!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Matty yaani kweli mjini shule.

Kuna baaadhi ya watu kutokana na ugumu wa maisha sasa wanaanza kuwa wasanii wanataka kutuletea ya Kibwetere

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Kitururu yaani kweli mkuu hapa kazi ipo.

Dogo kaona shule haina mchongo bora kuhubiri injili.Anasahau hata hao wamisionari wenyewe walikuja na kutujengea seminari ili watu wafunue mbongo zao..ila tutafika tu

Anonymous said...

Hapo sasa Kibwetere kachoma kanisa na waumini ndani sasa hawa sijui wana mpango gani??
Lakini nilisikia kuwa walitimuliwa mazingira ya Airport, sasa sijui walikoelekea!may be ni siku za mwisho, u never know!

Nalitolela, P. S. said...

duh!! Aisee hawa wamissionari wenyewe kwao dini 0; walisikia wapi Mungu anasaidia bila kujishughulisha. Yaani Visa huna, passport huna; hujishughulishi kuomba michango ya tiketi, halafu unategemea Yesu akushushie!? Huku ni kudata.

By the way, huyo dogo yuko 16!? Mbona anaonekana kama ana miaka 12

Anonymous said...

NDAKI mwe sijawahi pitia huku kwako ndo leo...WASABATO MASALIA vitukooooooooooooo