Friday, October 17, 2008

PUMZIKA KWA AMANI - NDALIMA Yusuph

Marehemu Ndalima Yusuph Nzaro -RIP

Picha ya ajali iliyotoa uhai wa rafiki yetu.

Nimesoma habari hii ya kusikitisha kutoka kwenye blog ya Issa Michuzi.
Binafsi sikubahatika kufahamiana na marehemu,ila nikiwa binadamu,kijana na mtanzania mwenzake hakika nimeumia sana.


Hakika kama maandiko yasemavyo huwezi jua siku wala saa ,kweli mauti tunatembea nayo.Hivyo ni vyema tutumie vema wakati wetu kwa kujiandaa na safari yetu.


Ndalima akiwa anasubiri taa za kuongozea magari ghafla anavamiwa na gari la mtoto aliyeiba kwako.

Na kwa wale wenye kuendesha vyombo vya moto tuwe makini ili tusiweze "kuwasababishia wengine mdahara ua kujisababishia sisi wenyewe madhara.


Pole kwa familia,marafiki na watanzania kwa ujumla kwa msiba huu wa mpendwa wetu uliotukuta.

Tuzidi kumwombea Ndalima apumzike kwa amani.Amina

Habari zaidi kuhusu ajali yake soma HAPA


RIP-Ndalima Yusuph.

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Ijumaa njema nawe pia= Trevligt helg (Kiswid)

Yasinta Ngonyani said...

ooh nilikuwa sikuona kuwa ndalima katuacha kulikuwa na kicha cha habari ijumaa njema. Basi nabadili nami nasema pia pole sana wanafamilia wote. na tumwombee marehemu astarehe kwa amani. Amina

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yaap Yasinta ni habari ya kusikitisha sana kijana mwenzetu ndio katutoka.

RIP Ndalima

Anonymous said...

mwenyezi Mungu aipumzishe roho ya marehemu mahala pema peponi.

RIP Ndalima

Anonymous said...

ni habari ya kusikitisha sana.

mwenyezi mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema penoni.

amina

zakaria

Anonymous said...

RIP Ndalima, yaani na mimi nilipata ajali ya gari the same day na huyu kaka nikajisemea moyoni Mungu atuponye mara moja, lol! kesho yake nasikia kaaga dunia , namshukuru Mungu mimi naendelea vizuri,i was appaled a lot.
RIP Ndalima!