Wednesday, October 15, 2008

KULIKONI Bongo Celebrity?


Picha ikionyesha mtandao wa Bongocelebrity.com ukiwa kimya.

Kwa muda wa majuma haya mawili kumetokea hali isiyo ya kawaida.Hii ni kutokana na mtandao ni upendao kutoweza kuendeleza libeneke.


BC ilikuwa ni miongoni mwa mitandao ambayo nilikuwa napenda sana kupita kila siku.Nimekutana na marafiki wengi sana wapya na wazamani.


Nimesoma hoja,michango mbalimbali ya wadau.Kubwa ya yote nimebahatikana kuona sura na matukio mbalimbali za mselebriti wa kibongo.


Kwa yoyote mwenye taarifa kuhusu timu nzima ya BC naomba japo kunidokeza nami nijue.


Mwisho nawamiss sana watu wangu woote.Gervas,Matty,Kekuu,mama wa kichaga,Chris,Any,Dinah,Any,Amina,Pearl,Olive,Halima,Binti-Mzuri,Ramla,Queen,Pendo,Kahindi,
manenn,Mzanzibar 100%,Hombiz,
mtajiju na wengine weengi ambao najua ukurasa hautatosha.

Nawaomba mwenye taarifa basi anistue.

siku njema watu.

TUTAFIKA TU

11 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mita kullo, ni kweli kaka Edo ulikuwa umepotea mchana mwema nawe

MARKUS MPANGALA said...

hata nashindwa kusema kwani naona kama wanaumwa kidogo labda!!!!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yasinta mimi mzima habari ya wewe?

namshukuru Mungu mambo yanaenda vema.

siku njema

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Markus sio kawaida yao kupotea kiasi hicho labda kuna tatizo.

mambo yanasemaje huko mkuu?

Anonymous said...

Aiseee nami nashangaa sana kwa BC kuwa kimya! Naamini Jeff atatoa angalau sababu ya BC kuwa "hush" namna hii!

Anonymous said...

Was wondering myself nikadhani ni mimi tu siwapati...wamekuwa mdebwedo kabisa may be kuna issue sio kawaida yao kabisa.
Mimi naona tutafika lakini kwa kuchoka!

Anonymous said...

Mi mwenyewe nashangaa mzee wa tutafika anyway tusubiri, Jeff atatueleza.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Chris nimefurahi kukuona tena japo kwa vidakika maana BC yetu sijui inahujumiwa na nani?

Ila matumaini soon Jeff atatuleta majibu.

karibu tena Chriss

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Matty umenichekesha kwamba tutafika kwa kuchoka...aa aaa aa

unajua BC ndio kibaraza chetu..wanakwambia hata kama una TV home lakini kutazama mpira ukiwa na company ndio unakuwa mtamu..

sasa Bc WANATAKA MIMI nibakie natazama mechi bila wadau...aa

tutafika tu

EDWIN NDAKI (EDO) said...

kekue..jamani karibu tena ingawa leo umenikuta nina haraka ndio maana hakuna hata maziwa ya kunywa..
karibu siku nyingine.

Anonymous said...

ahahahahhaahaha Edo ukweli ndo huo tutafika lakini kwa kuchoka!!! eti mpaka leo hawapo sijui imekuwaje walai!
Ukweli ni kwamba hakuna kama BC viwanja vingine vipo ila BC ndo our lovely ground!
Heeee ndo unamkaribisha kekuu bila hata soda basi maziwa hakuna na maji je???