Thursday, October 9, 2008

MAJAMBAZI YAVUNJA KANISA, YALA SAKRAMENTI


Hakika ukistajabu ya Musa utayaona ya Firauni.
Majambazi nane wamevamia na kuvunja kanisa la Hija la Bikira Maria la Mwanjelwa Mbeya na kuiba Sadaka,kompyuta,pesa na kisha kula sakramenti takatifu.
Kana kwamba hiyo haitoshi pia waliingia katika kituo cha kulea watoto yatima na kuibia pia.Watu nane wanashilikiwa kutokana na tukio hilo.
Habari zaidi bofya HAPA.
Hivi wazalendo tunaenda wapi sasa?Yaani watu wanavamia hadi nyumba za ibada?Hadi nyumba za Yatima?
TUTAFIKA TU

7 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Mungu wangu weee! hao kweli wamelaaniwa kabisa. Sehemu zote za kuiba mpaka waende kuiba kwenye nyumba ya mungu, sasa watakwenda kuungama wapi. Haya kaka Edo mimi nabadili nasema tutafika kweli?

MARKUS MPANGALA said...

Naomba kutofautiana na dadangu Yasinta kwamba wamelaaniwa. Vipi majuma kadhaa askofu wa kanisa la walokole amebambwa akijihusishwa na ujambazi huko mikoa ya kaskazini hapa bongo naye kalaaniwa? jamani vipi hali za maaskofu na watumishi wa mungu kutapeli? alaah kumbe wameiba kanisani! na hao wanaotoka kanisani kutuibia raia? hili suala siyo kwamba tutashindwa kufika ila tunatakiwa kutumia akili zetu na kujihoji kama kweli dini ndiyo mhimili pekee ambao unaweza kujenga maadili ya wanadamu! Ni kweli kwamba hizo ni nyumba za mungu? mwenyewe mungu kasema hivyo? vipi wale waliompigia kura Joji kichaka kwa sera yake ya God,Gay and Gun? aliposema God alimaanisha mashirika ya dini kupinga ushoga lakini walijua kwamba anakwenda huko Irak kufanya mambo, tulisema nini? vipi makanisani kwenyewe kuendeshwa na mashoga? tena kanisa anglikana huko uingereza? dini zinasemaje kuhusu mahusiano ya jinsia moja?je ni kweli huu ni utamaduni wa mwafrika? ni kweli mwafrika hakuamini kuhusu mungu mpaka wakaletewa haya makanisa? wapi ilipo afrika leo kama hao walioneza hizo dini wanatengeneza mabomu na kuua watu? mbona pale Palestina na Israel twasema huko ni nchi takatifu? utakatifu huo uko wapi kwa kumaliza maisha ya wapalestina? ni kweli kwamba dini ndiyo kila kitu katika amisha ya wanadamu? kaka Edo hakika waafrika kazi tunayo, kwani Maprofesa wao huko ughaibuni wanapotosha(soma katika blogu yangu angalia video ya Daily motion) historia ya waafrika weusi na kuibeza lakini tunajaribu kuwauliza chanzo cha ustaarabu wa afrika wanakijua? mbona yule Mtawa PLACID TEMPEL aliandika kitabu cha BANTU PHILOSOPHY kwamba tunamini dini za jadi ambazo ni sahihi?huyu alikuwa Kongo DRC alikuwa mtawa wa kibelgiji. Je kweli dini hizi ni kila kitu? sawa sote tumetoka kwa adamu na hawa, ikawaje tukatenganishwa ikiwa mungu wetu mmoja? wahindu,wabudha vipi? ni kwa hakika gani kwamba mungu ameegemea katika dini fulani? mmm jamani hivi najieleza vizuri? ngoja nikomee hapa salamu kwa dada Yasinta Ngonyani i love u my sister, be blessed. kitabu cha AMERICANA ENCYCLOPEDIA Vol. 10 KIMEANDIKA HISTORIA ZA WEUSI KWA UPOTOSHAJI TU.eti weusi hawana lolote katika ulimwengu. someni hapo DAILY MOTION

MARKUS MPANGALA said...

jamani huu ni mtazamo tu wala msikasirike washkaji haya mawazo tu.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Markus asante kwa machango wako mpana na mrefu.


Ni kweli tuna mengi ya kujifunza kwenye haya yanayoendelea na kusoma alama za NYAKATI.

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Yasinta watu wameshakata tamaa.

Kinachofuata ni falsafa za Darwings ..mwenye ubabe ndie atakaye survive.

Yaani wanaenda kuwaibia hadi yatima.

eehe..Mola wasamehe..maana WANAJUA wanayotenda.

Anonymous said...

Amebarikiwa yule amtumainiaye Mungu kuwa Mwokozi wake!sidhani kama adhabu yao wezi hao inafutika milele!na kwa yatima viumbe dhaifu wa Mungu poleni sana Mungu awape nguvu na awalinde!
Inatia uchungu sana, iko siku Mungu atasema nao wezi!

MARKUS MPANGALA said...

je kubarikiwa kwa mabeberu wanaopora mali za afrika mungu haoni? alaah kumbe nimekumbuka tunawaachia wenyewe. lakini kweli mungu ni mwokozi wetu tena sana lakini siyo lazima kufuata itikadi za mababu wa mashariki ya kati. na je mungu pale palestina anambariki nani jamani? alaaha kumbe naingia katika siasa samahani sijakata tamaa ila tutafute ukweli kuhusu imani na wezi hawa wanyongwe au tusiwanyonge?