Sunday, January 18, 2009

ZIMBABWE YACHAPISHA NOTI YA "TRILLION 100"


Zimbabwe Dola milioni hamsini.


Zimbabwe hali inazidi kuwa tata kiuchumi na kijamii.Kutokana na uchumi "kupoteza" mwelekeo serikali ilifyatua noti ya bilioni 50.


Hali imezidi kuwa mbaya majuzi wamefyatua trilioni 100 sawa na US dola 30.


Wanao pata tabu ni rai wa hali ya chini....

Baba Mugabe na wapambe wenu kubalini jamani yaanishe..Mtachapisha pesa mpaka mwishowe mtaona haisaidii bora mrudi kwenye biashara ya kubadilisha vitu..


6 comments:

Anonymous said...

Tanzania mambo yetu bado ni magumu,lakini ukiangalia Zimbabwe ndio tunaona kumbe tuna afadhali.

JK TUMUOMBEE ajitahidi kurekebisha uchumi tusije kufika huko


zaka.a towan

Anonymous said...

Hivi viongozi wa afrika mbona vichwa maji walio wengi?

Mugabe anataka kufia madarakani.Museeni alijitahidi kubadili katiba akashindwa.

haya ngoja ya mkute ya SIERRA LEONE

Anonymous said...

Duh hii kali yaani hapa Uk ina maana ukienda na trillion mia hupati hata jeans...aaa aaaa

Afrika pole sana

Anonymous said...

Wazungu waonevu tu.Mi namkubali sana Mugabe...

Sema hii dunia ya leo wachache ndio wanaongoza uchumi wa dunia ndio maana wanaamua dola ya zimbabwe ishuke thamani...

Mugabe fyatua sana minoti ukikosa ya karatasi toa hata ya plastic..tee teeee

John Mnyika said...

Ni madhara ya uongozi mbovu

Mnyika

EDWIN NDAKI (EDO) said...

John asante sana kwa kupitia hapa kwenye basi letu linalosafiri.

Hakika utawala mbovu ni mmoja ya vyanzo vya umaskini uliokithiri,vita,rushwa n.k

tupo pamoja