Wednesday, February 18, 2009

MCHUNGAJI WA KANISA LA PENTEKOSTI AKAMATWA NA VIUNGO VYA ALBINO

Mchungaji wa kanisa la Pentekoste mkoani Mbeya wilaya ya Mbozi Idiwili,Cosmas Mwasenga (39) na Luseshelo Mwashilindi (38) anakamatwa na jeshi la polisi kwa kukutwa na viungo vya binadamu.

Mchungaji huyo alikuwa akiviuza na ndipo polisi walipopata taarifa walijifanya kama wao ni wanunuzi na kisha mchungaji kuwaonyesha viungo hivyo.

Mchungaji alikuwa akiviuza kwa gharama za shilingi milioni 30.Viungo hivyo ambavyo ni sehemu ya mkono vimepelekwa kwa mkemia mkuu wa serikali wakati taratibu za kuwaburuza mahakamani zikikamilika.

Habaza zaidi bofya hiyo linki  Dullonet.com

Duh hii hali sasa inatisha..kama hata baadhi ya viongozi wa dini nao wamekuwa hivi.

Ila naamini mambo yatakuwa sawa..

Tutafika tu

3 comments:

Simon Kitururu said...

Sasa sijui tunaelekea wapi!:-(
Lakini kama usemavyo, TUTAFIKA TU!

Anonymous said...

Poleni na majukumu! kwa habari kutoka kwa kiongozi wa makanisa ya kipentekoste kutoka eneo la tukio amekaririwa na vyombo vya habari kusema kwamba ALIYEKAMWATA SIYO MCHUNGAJI WA KIPENTEKOSTE, bali alikua mshirika wa kawaida na alikua na mazoea ya kwenda kuhubiri sokoni na kando mwa njia!kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE NA MWANANCHI YA LEO Katika Neno la Mungu tunasoma Shetani hujigeuza kama malaika wa nuru, amejiingiza makanisani hata watu bila kujua humuabudu! na ndiyo ilivyotokea kwa huyu kijana itakua kabisa alikua na lengo fulani, na wengi wanakuja makanisani sio kwa nia moja, bali wanakuja kwa maslahi yao binafsi, lakini Mungu sio mwanadamu siku zao sio nyingi hukamatwa kama ilivyotokea kwa huyo ndugu yetu. Mungu abariki kazi za mikono yenu!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Kweli simoni kufika lazima hata kama tutakuwa tumechoka