Friday, February 20, 2009

ALIYEKAMWATA SIYO MCHUNGAJI WA KIPENTEKOSTE




Poleni na majukumu! 

Kwa habari kutoka kwa kiongozi wa makanisa ya kipentekoste kutoka eneo la tukio amekaririwa na vyombo vya habari kusema kwamba ALIYEKAMWATA SIYO MCHUNGAJI WA KIPENTEKOSTE, bali alikua mshirika wa kawaida na alikua na mazoea ya kwenda kuhubiri sokoni na kando mwa njia!Kwa mujibu wa gazeti la NIPASHE NA MWANANCHI YA LEO .

Katika Neno la Mungu tunasoma Shetani hujigeuza kama malaika wa nuru, amejiingiza makanisani hata watu bila kujua humuabudu! na ndiyo ilivyotokea kwa huyu kijana itakua kabisa alikua na lengo fulani, na wengi wanakuja makanisani sio kwa nia moja, bali wanakuja kwa maslahi yao binafsi.

Lakini Mungu sio mwanadamu siku zao sio nyingi hukamatwa kama ilivyotokea kwa huyo ndugu yetu. Mungu abariki kazi za mikono yenu!


Ufafanuzi huu umetumwa na Dada Mary Damian ambaye unaweza kumtembelea kwenye blog ya Gospel kwa kubofya HAPA




No comments: