Tuesday, April 14, 2009

nipokeeni:NIMEREJEA NA NGUVU MPYA!!


Kamtambo kapya Canon EOS 1000D

Habari za madeisi kadhaa wapendwa ambao wote tupo safarini.

Kwanza naomba kutumia nafasi hii kuwaomba msamaha kwa kushindwa kuaga au kupandisha mtundiko.

Namshukuru Mungu kwani ni mzima wa afya na nimerejea na nyenzo mpya kwa ajili kutuwezesha kufika tu!Upande huu wa ufini kajua ndio hakooo kameenza kujichomoza na kuashiria shamra shamra za majira ya kiangazi "suma" ndio sasa..

Karibu kunitembelea huweze kujionea vimbwanga,matukio habari za ufini na sehemu mbalimbali za kona za dunia..

Naamini tupo pamoja na tutafika tu...
Asanteni sana wadau mbalimbali ambao mmekuwa mkiwasiliana nami kuendeleze libeneke..hakika mnanitia moyo na nina amini sipo peke yangu

Tutafika tu

6 comments:

Yasinta Ngonyani said...

Karibu sana ni kweli ulikuwa umeadimika kweli.

Mzee wa Changamoto said...

Kaka. Karibu saaana. Japo nasi twasuasua kutokana na majukumu, lakini tunasonga taratibu. Tulikukumbuka na tulikutakia "mrejeo" mwema.
Na sasa kwa kuwa umerejea, tunasema kwa mwendo wowote utakaokuwa nao usituache namna hii. Maana majukumu ni mengi, muda mfupi, jamii ni kubwa na mtekelezaji ni wewe tuu. Lakinii.............TUTAFIKA TUUUUU

Christian Bwaya said...

Karibu sana kaka. Ninategemea kupata mambo makubwa zaidi...

Masangu Matondo Nzuzullima said...

Nimekaona kamtambo kapya. Ni enzi za nguvu mpya, kasi mpya, mtambo mpya...Karibu tena ulingoni.

Simon Kitururu said...

Mkuu Karibu!

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Edo umekimbia tena?