Sunday, May 10, 2009

MAMA POLENI!!! TUTAFIKA TU!

Picha ya wakinamama wakitoka kusaka maji.

Leo ni siku ya maalumu ya wakinamama duniani kote!

Nimeona nitumie muda huu kuwakumbuka kuwaombea wakina mama wote duniani waliotangulia mbele ya haki mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahala pema peponi.Amina

Nawakumbuka pia siku ya leo wakina mama wote walio katika mazingira magumu;Walio katika maeneo ya vita,wakimbizi na wale wanaoishi chini ya mstari wa umaskini.Poleni sana hapo peke yenu.


Nilikuwa na hamu kama mngeweza kusikia sauti yangu au kusoma salaam zangu ila najua itakuwa ngumu kuyapa haya ninayotaka kutoa.

Kikubwa tuwakumbuke wakinamama woote waliokatika mazingira magumu na kuwasaidia kukabiliana na ugumu wa maisha.Ni wajibu wetu.

Happy mothers day!

Tutafika tu!!

Tutafika tu

1 comment:

Yasinta Ngonyani said...

Kaka Edo! ni kweli kabisa kina mama wanahitaji kupongezwa. Kunahitajika kufanya kitu ili sauti za akina mama zisikike,. Ningependa unyanyaswaji,kuwadharau akina mama ukomeshwe. Natamani nienda sehemu kama juu ya mlima kilimanjaro na kuitangazia dunia yote haki za akina mama hapa duniani. Nami namaliza kwa kusema TUTAFIKA TU!