Saturday, May 23, 2009

NANI KIDEDEA "SUMMER" HII?

Bongo FC yenye makazi yake jiji la Helsinki -Ufini
Timu wabongo ya TAS yenye makazi yake jiji la Tampere.

Mwaka 2008 TAS(tampere) ilitoa kipigo kwa bongo FC nyumbani kwao Helsinki na katika mechi ya marudiano iliyofanyika Tampere, Bongo Fc nao waliweza kuifunga TAS japo kwa mbinde(ukweli si unajulikana..aa.aaa)

Mbali na mchezo wa mpira ndio kipindi ambacho watu wengi huweza kukutana na kufahamiana kuburudika kubadilisha mawazo ikiwa ni sehemu ya utamaduni wetu(amani).

Kubwa ya yote inakuwa wakati mwafaka kwa Bongo FC kuweza kula nyama(maana wakikosa nyama inakuwa 'ishu'(nahisi gharama za nyama helsinki zipo juu sana..sina uhakika..aaa.aa )

Itabidi nimtafute Kocha wa Bongo FC atueleze kusuhu kesi ya pilau uswidi.

Nawatakia kila kheri katika maandalizi ya mashindano mbalimbali.Tuendelee kutumia michezo kama njia moja wapo ya kutuweka karibu kwa amani na upendo.

Tutafika tu








7 comments:

Anonymous said...

zile kalimati zenu ndaki zilikua na mchanga mwaka jana.

Anonymous said...

Tas mmechooka,mtaweza mbinde za Bongo fc?

Anonymous said...

aaa..bongo FC safari lazima mtawafunga maana wakenya waliokuwa wanawategemea wameanzisha timu yao..


Ndaki msiogope

said sweden said...

tas na bongo fc mnacheza makida makida moto wenu kilimanjaro fc..

tunakuja huko kugawa dozi tu

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Jamani TAS inatisha hasa ukichukulia vijana wapya waliowasili kwa ajili ya kuongeza ngumu.


mjiandae kwa kichapo safari hii

Anonymous said...

Bongo Fc tunamaliza msimu tampere, kwa hiyo wembe ule ule kama mwaka jana, mkumbuke kule kirputori wanauza makapu bei rahisi sanaaaaaaaa!!!!!


Mdau Guuus Hiddinho.

Anonymous said...

Tampere hamjakoma bado?, hangover ya kile kipigo cha bao tano naona bado mnayo.
Subirini masika ya magoli mwaka huu.

Bongo Fc Damu.