Monday, September 7, 2009

England yatinda Fainali 2-1

Mshambuliaji wa timu ya wanawake ya taifa la Uingereza Lianne Sanderson ambaye alikuwa moja ya chachu ya ushindi kwa mchezo wake mzuri kama nilivyomnasa na kidakio changu
Sina story ..ndege tunduni ndani ya lango la Uingereza
Kuteswa kwa zamu..Beki wa timu ya Uholanzi Bito akinyofoa samaki aliyenasa nyavuni na kuandika goli la pili kwa uingereza.
Sikuwa na moyo wa kwanini..Ilibidi niwashangilie wakoloni wangu(Uingereza)maana nchi yangu michezo ilienda na politiki kwa kuyumbisha "michezo mashuleni" nakuimarisha chipukizi..

Mpaka mwisho wa mpambo Uingereza 2-Uholanzi 1.Kwa maana hiyo Uingereza wamapeta tiketi ya kutinga fainali ambako itacheza na mshindi wa leo jioni kati ya Ujerumani au Norway.

Tutafika tu

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Asante kwa "nyepesi" hizi. Nilichofurahia zaidi ni kuwa UMENASA PICHA HIZO KWA KINASIO CHAKO.
Yaani Copyright ya @tutafika2009.
Kaka. Kazi njema na tuko pamoJAH
Blessings

Yasinta Ngonyani said...

Ni kweli taswira nzuri sana Edo. naona ulikuwa na wakati mzuri safi sanaaaa.

Anonymous said...

Thats ggod edu,upo juu na kiblog chako!

EDWIN NDAKI (EDO) said...

Asante sana wazalendo..Kwa kweli mechi ilikuwa nzuri sana..Itabidi nisafiri Alhamisi hii niende Capital city yetu Helsinki kwa kitururu ili kuweza kushuhudia Fainali