Nelson Mandela akiwa na Rais wa Rwanda Paul Kagame.
(Picha na Denis Farell)
Leo Oktoba 23 ni "birthday" ya rais wa Rwanda Paul Kagame.Alizaliwa mji Gitarama,Rwanda october 23,1957.
Akiwa na umri wa miaka(2) alikimbia yeye na familia yao pamoja na familia zingine za kabila la watutsi Uganda baada ya mauji yalioendeshwa na serikali ya wahutu nchini Rwanda.
Kwa zaidi ya miaka 30 aliishi ukimbizini nje ya nchi yake.Kwa msaada wa rafiki yake(Rais Yoweri Museveni) aliweza kuanzisha harakati za Rwandese Patriotic Front
April 6,1994 ndege iliyokuwa imembeba rais wa Rwanda Juvenal Hybarimana na rais wa burundi Cyprien Ntaryamira ilidunguliwa katika anga la Kigali,Rwanda.Kulipuliwa kwa ndege hiyo ilikuwa kama ndio mwanzo wa mauaji makubwa ya kimbali "RWANDA GENOCIDE"
Kwa siku mia moja zaidi ya watutsi na wahutu wenye msimamo wa wastani kati ya laki nane na milioni moja wanakadiriwa waliuawa.
4 July 1994, Paul Kagame na RPF wanafanikiwa kuwazidi nguvu utawala wa kihutu ulioongozwa na Jean Kambanda na kurejesha hali ya utulivu.Wanamgambo waasi wa kutoka kabila la wahutu Ntarahamwe hatimaye wanakimbilia Congo.
Kwa kifupi huyo ndio mtu ambaye kwa baadhi yao ni shujaa ila kwa wengine ni kinyume chake.
Binafsi namtakia maisha mema na marefu katia kurejesha mahusiano zaidi kati wahutu na watutsi na kujenga Rwanda mpya.
Happy birthday Paul Kagame!
1 comment:
Hongera Rais Paul Kagame kwa siku ya kuzaliwa.
Post a Comment