Wakili Emmanuel Tamira Makene akiwa na mke wake bi Sarah Twilumba muda mfupi baada yakufunga pingu za maisha.
Picha kutoka blog ya Issa Michuzi
Leo wakati nikitafuta nini cha kuandika ghafla nakutana na picha ya school mate wangu akimeremeta.
Bwana harusi ambaye kwa sasa anamiliki kampuni yake binafsi ya uwakili ya Kings Law Chamber.Kabla ya hapo alikuwa wakili wa magazeti ya serikali ya Tanzania Standard news paper.
Kwa kifupi huyu mheshimiwa ni miongoni mwa walinitupokea seminarini tukitafuta wito wa upadre,yeye akiwa kidato cha tatu mimi ndio "nyoya",bazoka, fomu wani.
Kwa mfumo wa seminari mara nyingi kidato cha tatu ndio wanakuwa wapo karibu sana na kidato cha kwanza kuliko kidato cha pili.
Kwa wale wanajua maisha ya shule nyingi za bweni za miaka hiyo kidato cha pili wao ndio "Military police"MP wa shule.
Bwana harusi alikuwa katibu wetu wa Debate club.
Binafsi nimefurahi na ninafurahi kuona watu ninao wafahamu wakiendelea kupiga hatua flani flani katika maisha.Namtakia kila la kheri katika maisha ya ndoa.
Unakumbuka nini kuhusu maisha ya shule?



0 comments:
Post a Comment