Wednesday, February 17, 2010

KITUO CHA WATOTO UPENDO DAIMA- MWANZA


Timu ya watoto upendo Center (Kati)

Timu ya Upendo Daima -Malimbe.
Napenda sana michezo hizo zilikuwa timu za watoto wetu ambazo nilikuwa nazifundisha soka.
Hakika kwetu ilikuwa zaidi ya mpira tulifurahi na kusahau shida zetu na huku afya zetu zikiboreka zaidi.Nawamiss sana watoto wangu wapendwa.

Dec,2004
Edo wa kwanza kulia nikiwa Bw Hoja pamoja watoto wetu wanaoishi katika mazingira Magumu
wilayani Geita mkoa wa Mwanza.Hapo tulikuwa tumeenda kwenye hiyo wilaya kufuatialia wapi walipotokea watoto hao na kuangalia uwezekano wa kuwaunganisha na familia zao.Kwani moja ya lengo letu kuu si kukaa na watoto kituoni kwetu bali ni kuwaunganisha na jamii zao.


Hiyo ilikuwa moja kazi zetu na maisha yetu kuwaondoa watoto wanaoishi mitaani nakuwaunganisha na familia(wale wenye familia zao) na wengine kuwalea katika kijiji chetu(Upendo Daima Children Center -Mwanza) kuwapatia elimu na ,faraja na upendo.

Kwangu haikuwa kazi bali ilikuwa ni wito niliopenda na Mungu akipenda karibuni nabeba mabegi yangu nikimaliza yaliyonileta huku narudi kuelendelea na pale nilipoishia.

Nawe kwa nafasi yako unaweza kufanya mengi popote ulipo ktk kuWAPA FARAJA WANAOHITAJI.

Tutafika tu.

3 comments:

John Mwaipopo said...

tuwapende watoto. watoto hawana hatia. pongezi kwa kazi nzuri ya kuonyesha upendo kwa walioukosa

Masangu Matondo Nzuzullima (MMN) said...

Ujumbe mzito. Tendo moja jema kwa binadamu mwenye uhitaji linaweza kuleta faraja isiyo na kikomo, likaweza kubadilisha kabisa mwelekeo na mtazamo wa maisha yake.

Najua kwa sababu tendo moja kama hilo lilishawahi kubadilisha mtazamo kuhusu wajibu wangu kama binadamu hapa duniani. Tazama hapa:

http://matondo.blogspot.com/2010/02/siku-niliyokutana-na-ubinadamu-wa-kweli.html

Yasinta Ngonyani said...

Pongezi kwa kazi nzuri. Ni mfano mzuri ambao unastaili kufuatwa na wengi. Ahsante. Na kweli Tutafika tu. Upendo Daima.