Sunday, July 25, 2010

Tunajifunza nini kutoka FINLAND?


Rais wa Ufini(Finland) Bi Tarja Halonen.

Waziri mkuu wa Ufini Bi Mari Kiviniemi.


Waziri Mkuu akiwa katika pozi lake nje ya majukumu.


Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa Tanzania.Kuna mambo mengi tunaweza kujifunza pia kutoka kwa hawa ndugu zetu wafini.Finland imepiga hatua kubwa kimaendeleo.

Imetajwa na shirika la Transparency International miongoni mwa nchi 6 bora zinazoongoza katika kupambana na rushwa duniani huku ikiendelea kupiga hatua pia.

Tunapoelekea kwenye uchaguzi,lazima tukubali kubadilika na kuchagua watu wenye uwezo wa kuotuletea maendelea na si kubakiwa na mitazamo ya kizama na kimfumo dume kwamba "mwanamke hawezi" kitu ambacho katu sikubaliano nacho.

Imefika wakati tukubaliane na maneno anayotumia dada yetu Mija Shija Sayi kwenye blog yake,kwa kuwaita wanawake wa shoka. Ukitaka kupata mambo kuhusu wanawake washoka basi bofya hilo jina hapo la huyo dada yetu.

Ni mtazamo wangu,kuwa yoyote mwenye uwezo na nia basi anatufaa kuwa kiongozi na sio suala la kuangalia jinsi ya mtu.

Tutafika Tu!

5 comments:

Subi Nukta said...

Napata faraja kukusoma Eddo kuwa umeifuta dhana ya kuwa, jinsia/jinsi lazima ivikwe majukumu na shughuli fulani fulani. Imefika wakati tukubali kwa videndo ile kauli ya kuwa, 'binadamu wote ni sawa' la sivyo tutakuwa tunadanganyana na bora tuache kusema hivyo. Yeyote anayetaka na apewe, akishindwa ataachia au ataondolewa. Tusiwazuie watu uwezo wao kwa vigezo vya jinsi/jinsia, rangi ya ngozi, kimo, kabila nk.
Asante!

Yasinta Ngonyani said...

Kwa kweli ni furaha kuona wanawake wanaanzas kuchukua nafasi. Haya ndio mambo yanayotakiwa kuigwa. Kwani kujishusha shusha kuishe sasa na iwe watu watu tu sawa na kwamba wanawake tunaweza. Sawa kabisa wanawake wa shoka.

Simon Kitururu said...

Mmmh!

Maisara Wastara said...

Safi sana kua na wanawake wa shoka kama hawa wa Ufini

Yasinta Ngonyani said...

Edo upo wapiiiii????