
(Enzi za uhai wake msanii Abel Motika aka Mr Ebbo)
Nilipumzika kuandika lakini kwa hili la rafiki yangu Abel Motika(Mr Ebbo sasa narejea kublog ingawa naanza kwa post huku moyo wangu ukiwa umeumia lakini yote mapenzi ya Mungu.
Msanii wa kizazi kipya na Producer Abel Motika aka Mr Ebbo kaaga dunia jana December 1,2011.
Mr Ebbo mbali na usanii pia alikuwa na studio yake binafsi iliyokwenda kwa jina la Motika Records.
Binafsi nilimepokea kwa masikitiko na mshtuko msiba wa Mr Ebbo.
Alikuwa rafiki yangu nikiwa nasoma Eckernforde High School mkoani Tanga wakati huo Mr Ebbo yeye akijishughulisha na shughuli zake mpaka alipotoka kwenye game na album yake ya FAHARI YAKO huku ikiwa na nyimbo kama vile mimi mmaasai kibao kilichoweza pendwa sana kipindi kile.
Binafsi namkumbuka Mr Ebbo jinsi alivyokuwa mcheshi na mtu wa watu.Mara ya mwisho tulionana 2005 Dsm mitaa ya sinza kwa Remmy tukapata "supu ya mbuzi".Sikujua kuwa ndio nilikuwa naagana na Abel Motika.
Bado nakumbuka uliponiambia "kaka ukirudi kutoka ufini karibu motika Record uingize sauti hata kama utatoa track hata kama itakuwa mbofu mbofu" naamini unaweza.Asante nilichelewa kuja lakini ushauri umefanyiwa kazi.
Pumzika kwa amani Abel Motika aka Mr Ebbo.Pole kwa familia,ndugu jamaa marafiki.
Wewe umetangulia nasi tutafuata.Amina
2 comments:
Nilitaka kushangaa na tena kusikitika sana kama usingesema kitu kwani ni hisia zangu tu kuwa mlikuwa marafiki...Pole kaka Edo. Nami vivyohivyo nilipatwa na mstuko wa ajabu niliposikia kwani mr. Ebbo nyimbo zake zimetawala katika nyumba yetu. USTAREHE MAHALI PEMA PEPONI.
KAKA EDO KARIBU SANA SANA TENA BINAFSI NILIKUWA KARIBU KUKUTANGAZA KUWA UMEPOTEA NA TUKUTAFUTE.
Asante sana Dada Yasinta.Hakika kweli nimepotea.Ila hata leo hii nilipita kuomboleza pamoja na jumuiya yetu ya bloggers.
Bado najipanga kuna mengi sana yametokea kwenye kuadimika kwangu lakini lakini tupo pamoja.
Kila siku nimeweza kuchungulia not less than 10 blogs yako ikiwa mojawapo,na ninafarajika kwa jinsi unavyoendelea vema kublog.
Mungu akitujalia uzima nitarejea na simulizi na picha nyingi kuanzia dec 20.Tuzidi kuombeana nipate nguvu ya kurejea kublog..Nifikishie salaam zangu kwa marafiki wa zamani blogger/wasomaji,waambie karibu nitareje.
Tutafika tu
Edo
Post a Comment