
Wakazi wote wa Finland hususani mnaoishi jiji la Tampere.
Kundi la "Pagan Front" linakusudia kufanya tamasha lao leo katikati ya jiji, jirani na kituo cha mabasi-Keskustori.
Tukio lenyewe litafanyika kwenye mtaa wa helmikuuta Tampereen Yo-talolla ja 2.
Watu weusi,wameombwa kuchukua tahadhari ya kutosha kwani wafuasi wa dini hiyo pia wanaweza kufanya vitendo vingi vya Kibaguzi dhidi ya watu weusi.
Jambo linalo hofiwa uenda kukatokea na vurugu ni kutokana na sheria za ufini kupiga marufuku miziki inayoendana na chama kilichokuwa kikiongozwa na Adolf Hitler cha Nazi Party.
Kwa habari zaidi soma...
http://nspublishing.wordpress.com/2008/01/03/pagan-front-concert-in-finland/
4 comments:
pamoja kamanda poleni sana na hao wajinga jinga.
Ubaguzi bado upo kwenye dunia hii.
hio rangi haina ustaarabu wa aina yoyote
Ndaki asante sana kwa kutustua.Maana mimi nilikuwa sina taarifa kabisa.
Pamoja ndugu yangu.
Ndaki umekumbuka kijiwe chako eeh, maana kutwa uko kwenye vijiwe vya wenzio, yaani kila siku ukiingia kwenye blogu yako ola hakuna kitu lakini tunakuona kwenye blogu nyingine. Hebu tupe vitu vya ufini maana waswahili wanasemaga barua ni nusu ya kuonana. Sasa wewe ukipost humu mambo ya ufini itakuwa kwetu ni nusu ya kuiona hiyo ufini.
Turudi kwa hawa watu wasio na roho wala ubinadamu, yaani mie wananichosha hasa kwa tabia zao za ajabu. Lakini utashangaa sie waswahili tunavyowapapatikia. Sisemi na sie tuige tabia zao mbaya lakini tuwe makini.
Ujue mtu mweusi ndio wa kwanza kustaarabika duniani halafu ndio wakaja hawa. Ukisoma black history kwa undani utaelewa vizuri.
Mama Malaika
Post a Comment